Habari ya Asubuhi. Unaendelea Vyema! Mwaka bado haujaisha bado unayo Nafasi ya kuleta mabadiliko kwenye Mwaka huu 2016. Siku chache zilizobaki unaweza kuacha alama. Unaweza kufanya kitu ambacho hautakaa ukisahau.
Kuna watu walikua wamekata tamaa wakaniomba Ushauri nikawaambiwa waanze biashara mwezi huu huu. Wasisubiri January. Hivyo hata wewe unaweza kuanza kitu leo na ukafanya maajabu.
Ulishawahi kusikia mtu anakwambia kua chanya au fikiri chanya?  Ukifikiri chanya haimaanishi wewe utakua unaweza kila kitu. Yaani kwa kufikiri kwako chanya hakukufanyi uweze kushinda mpira kama hujafanya mazoezi. 
Kwa kufikiri chanya hakukufanyi uweze kwenda kumtibu mgonjwa wakati wewe ni Mwalimu. Kwa kufikiri chanya peke yake hakukufanyi wewe uweze kufanya kila kitu.
Kufikiri chanya kunakufanya wewe uweze kufanya vizuri zaidi. Kufikiri chanya kunakufanya uweze kusonga mbele kwenye kile unachofanya.
Usishangae ukianza biashara fulani mpya na ukawa na mategemeo mazuri sana lakini ukafeli. Hiyo inatokea kila Mahali. Kushindwa hakumaanishi wewe hufikiri chanya bali kuna vitu hukuviweka sawa. Au hicho ukifanyacho hakiendani na wewe.
Bonyeza hapa kupata Zawadi niliyokuandalia Christmas na Mwaka Mpya ….  http://subscribe.jacobmushi.com/g7r0z1
Karibu sana kwenye semina itakayofanyika kwa njia ya mtandao mwanzoni mwa Mwaka 2017. Mwisho wa Kujiunga ni tarehe 30/12/2016 Tuma Neno Semina kwenye no 0654726668 kupata maelezo zaidi
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: 0654726668
Email: jacob@jacobmushi.com
Blogs: www.jacobmushi.com & www.jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading