FANYA HAYA USONGE MBELE KIBIASHARA

jacobmushi
By jacobmushi
3 Min Read
Unapohamia kwenye jengo jipya tunaweza kusema biashara yako imekua lakini ukweli halisi sio huo,  biashara haikui kwa wewe kuhamia kwenye jengo kubwa au kubadili usafiri.  Leo tutakwenda kuona jinsi gani unavyoweza kukuza biashara yako.
Kuna aina mbili za kufanya biashara yako ikue.
1. Idadi ya wateja kuongezeka
Tuseme mwaka jana ulikua unahudumia wateja 50 na mwaka huu wameongezeka na kufikia 150 hapo tunasema biashara yako imekua kwa sababu wateja wameongezeka. Wateja wakiongezeka  na mapato yako kinaongezeka. Hivyo basi kama unataka kukuza biashara yako hakikisha wateja unaowahudumia wanaongezeka kila iitwapo leo.
2. Biashara yako inaweza kukua kwa kuongeza vitu unavyouza kwa wateja wako mfano kama ulikua unauza maji kwa watu 20 unaweza kuongeza ukawa unawauzia na bytes  labda na juice hapo biashara itakua japo ni kwa kiasi kidogo lakini mapato yataongezeka. Biashara yeyote unayofanya kama haikui ni tatizo. 

Ufanye nini ili kuongeza idadi ya wateja kwenye biashara yako?
– Hakikisha kila mtu mpya unaekutana nae anajua ni nini unafanya kwani anaweza kua mteja wako au akakuletea wateja wengine.
-Tumia mitandao ya kijamii kama WhatsApp, Instagram, Facebook, Twitter etc kutangaza biashara zako.  Kwa kupitia mitandao hii utakutana na watu sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi na kwa haraka zaidi.  Na hii ndio njia ya pekee ambayo haihitaji gharama kubwa.  Kitu kikubwa cha kufanya kwenye mitandao hii sio kutangaza biashara peke yake kitu kikubwa cha kufanya ni kujenga uaminifu kati yako wewe na wateja wako. Kutokana na wimbi la utapeli ni ngumu sana mtu kukuamini ukimwambia akutumie hela umtumie mzigo yeye yupo Arusha wewe upoa Dar.  Lazima kuaminiana kwanza kuwepo. Sio rahisi vile vile wewe umtumie mtu mzigo wako bila kukupa hela lazima kuwepo na uaminifu. Kukiwepo na uaminifu ndipo biashara inapoweza kufanyika.
Kama umeweza kusoma ujumbe huu na bado hujaanza unapoteza muda anza sasa sio lazima iwe biashara inawezekana ni hobby yako, ujuzi, taaluma yako anza sasa jenga mahusiano mazuri na watu ipo siku utaona matunda yake. 
Nikushukuru kwa kwa kusoma mpaka mwisho.
Kwa msaada na maelekezo zaidi wasiliana nasi kwa 0654726668, mojatechnologiesgroup@gmail.com 
Asante sana na Karibu.

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading