HATUA YA 12; Wewe Rafiki Yangu.

jacobmushi
2 Min Read
Wewe ni Rafiki Yangu hivyo lazima wakati wote niwe nakwambia Ukweli. 
Ukweli ni kwamba usipokubali kubadilika mwaka 2017 utakua mgumu zaidi.

Wewe Rafiki Yangu usiopoacha kuishi maisha yako halisi utaishia kuteseka moyoni mwako kwa kuwaridhisha wengine.
Wewe Rafiki yangu acha kuwa mzembe kila siku nakwambia kusoma vitabu ni muhimu sana lakini unahisi nakutania. Lakini ipo siku utaelewa kwanini nakwambia. Sitamani ifike hiyo siku kwako maana ni mbaya ni majuto ndio yatakufanya uelewe.
Wewe Rafiki Yangu kama hutokubali kuweka juhudi katika maisha yako usitegemee kabisa muujiza kutokea. Kile unachotamani kitokee kwenye maisha yako hakitokei kama muujiza lazima ulipe gharama ya kukipata na gharama hua ninakwambia kila wakati.
Wewe Rafiki Yangu nakwambia sio kila mtu ni wa kuambatana nae maana watakupoteza lakini bado hujanisikia. Wakati Ukifika utanielewa kwanini nasema hivyo. Wakati huo ni majuto na masikitiko. Sitaki kabisa ufike huko. Acha kupoteza muda na watu waliopoteza dira. Watu ambao hawajui wanapoelekea wanaotegemea matokeo wasiyofanyia kazi.
Naomba leo niishie hapa Rafiki Yangu. Napenda kukwambia kwamba Hamu yangu ni kuona unafanikiwa lakini wewe usipokubali kuchukua hatua hizi ili ufikie Mafanikio huwezi kufanikiwa.
Karibu sana.
Jacob Mushi. 
Entrepreneur & Author 
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418 
Email: jacob@jacobmushi.com 
Blogs: www.jacobmushi.com , www.jacobmushi.com  
jacobmushi.com.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading