Kuna msemo mmoja watu huwa wanapenda kuutumia mara kwa mara lakini ni utetezi tu wa tabia zao ambazo ni mbaya juu ya pesa. “Pesa Huwa Haijai hata Siku Moja” kwangu huu ni uongo na kujitetea tu ili undelee kuongozwa na tamaa zako. Kama wewe ni mtu mwenye malengo na maono huwezi kuutumia msemo huu. Kama wewe ni mtu mwenye nidhamu ya pesa huwezi kuutumia msemo huu.

 

Kama utaendelea kuutumia msemo huu maana yake ni kwamba utaendelea kuitumikia pesa hadi Maisha yako hadi unakufa. Kikawaida ili uifurahie pesa unatakiwa ufike katika hatua ambayo pesa itakufanyia kazi wewe na sio wewe unafanya kazi ili upate pesa.
Kama mtu unaejitambua lazima ujue kutofautisha vitu vya muhimu kwenye Maisha yako na vitu ambavyo vinaweza kusubiri au sio vya lazima kabisa. Hii itakuwezesha wewe ufikie malengo yako bila kuishia kulalamika kwamba pesa hua haitoshi wala kujaa.
Ili utoke kwenye gereza hili lazima uwe na malengo ya fedha labda baada ya miaka mitano unataka uwe unamiliki fedha kiasi gani. Kama ni kwenye biashara au kazi unayofanya basi uweke malengo. Bila hivyo hutajua unapokwenda. Hata pesa ukizipata hutajua unazitumia vipi.
Soma: Usioyajua Kuhusu Pesa Haya Hapa
Kama huna maono hutajua ni kwa kiasi gani unatakiwa uwe na nidhamu ya pesa ili uyafikie maono yako.
Ili utoke kwenye gereza hili kuwa na vipaumbele vya Maisha yako. Sio kila kizuri unachokutana nacho unakitaka. Sio kila kinachovutia macho yako unataka kununua. Bila kuwa na vipaumbele utajikuta pesa yako inapotelea kwenye vitu ambavyo wala huna kazi navyo.
Ili utoke kwenye gereza hili kwanza futa kabisa hayo maneno kisha anza kuweka akiba. Kama unaweka akiba lazima utakuwa umepiga hesabu zako jumla ya pesa utakazokuwa umekusanya kwa mwaka mmoja au baada ya miaka mitano. Hivyo pesa sio hazijai bali unaweza kuweka malengo ya kiasi gani cha pesa unataka na ukaanza kufanyia kazi hadi kukifikia.

 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading