Habari za Leo Rafiki na Mwanamafanikio. Ni matumaini kwamba unaendelea vyema na harakati za kufikia mafanikio yako. Siku zinakwenda kila siku, tarehe zinabadilika, majira yam waka yanabadilika, wewe unabadilika? Unasonga mbele? Kama hubadliki basi kuna tatizo mahali.

Leo tuangalie msemo ambao hutumiwa na watu wengi mara kwa mara BIASHARA NI MATANGAZO. Kweli biashara ni matangazo. Kwanini makampuni makubwa ambayo yapo kitambo sana kwenye chati hadi leo yanajitangaza redioni na kwenye televisheni? Unafikiri ni kwanini wanaleta promosheni kila wakati? Au unafikiri ni kwasababu tu kuna kitengo cha masoko? Ukweli ni kwamba biashara ni matangazo japokuwa soda ilikuwepo tangu nazaliwa hadi sasa ipo jina ni hilo hilo, ili wauze lazima wajitangaze.
Kwenye ulimwengu wa sasa kuna vitu vingi sana ambavyo vinachangangia watu wajisahau kutumia bidhaa yako. Haijalishi ni bora kiasi gani kama watu hawaioni ikisikika kwenye masikio yao sio rahisi wakafanya maamuzi ya kununua bidhaa yako. Changamoto nyingine ambayo ni kubwa sana ni kwamba kuna watu wengi sana sasa hivi wana biashara ambayo inafanana na yako. Kama hawapo basi wanaweza kuanza hata sasa na wakachukua wateja wako.
Hakuna namna nyingine watu watafahamu ile bidhaa yako bora kama huitangazi, haijalishi ni njia gani unatumia kutangaza lakini ili waifahamu lazima uizungumzie wewe au wateja wako wazungumzie ubora wake. Ukikutana na mtu analalamika hana wateja kwenye biashara yake muulize mpango wake wa masoko ukoje. Biashara nyingi ndogo ndogo zinatumia mfumo wa zamani sana wa kukaa kwenye ofisi na kusubiria mteja aje.
Dunia ya sasa imebadilika lazima uinuke ulipokaa utumie njia mbalimbali za kuinua mauzo yako. Ubunifu ni wa muhimu sana ili uweze kutengeneza picha nzuri ya biashara yako.
Mambo Ya Kuzingatia Kwenye Kutangaza.

Wateja UlioNao Sasa.
Wateja ulionao sasa ni sehemu ya kwanza ya kujitangazia. Kama ulikuwa hujui basi anza kujua leo kwamba kila unachomfanyia mteja wako ni tangazo tosha analopeleka kwa watu wengine. Kama utamhudumia vibaya basi ujue tangazo ulilopeleka kwa watu wengine ni baya. Sehemu hii ndio sehemu ya kuwa makini sana kwani inakufanya wewe uendelee kuwepo sokoni.
Haijalishi mteja aliekuja humfahamu mhudumie vizuri kwani hujajua ameelekezwa na nani. Vilevile hujui anamjua nani. Kama utaitumia fursa hii vibaya utajitengenezea kaburi mapema sana la biashara yako. Haijalishi biashara yako ni kubwa kiasi gani kama hujali wateja wako lazima watakutangaza vibaya.
KUMBUKA: Habari Mbaya zinasambazwa Haraka kuliko Habari njema.

Unatangaza Nini?
Haijalishi bidhaa yako ni bora kiasi gani Hakikisha unajua inakwenda kufanya nini kwa yule unaemuuzia. Tangazo lako linatakiwa libebe utatuzi wa shida ya mteja wako. Mteja akiliona tangazo aone shida yake imetatuliwa hilo ndio linamfanya afanye maamuzi.
Kuna wateja wananunua sio kwasababu ya bidhaa yako bali ni kwasababu wameona watu wamenunua.
#USIISHIE_NJIANI
Itaendelea….
Jacob Mushi
Mwandishi na Mjasiriamali.
Phone: +255654726668

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading