HATUA YA 169: Uhuru Wako Uko Hapa.

jacobmushi
3 Min Read
Kuna nyakati unaweza kujikuta una mambo mengi yamekufunga kwasbabu tu ulishindwa kutambua uhuru wako unapatikanaje. Inawezekana ulijifunga kwasababu ya maneno yako, au kwasababu ya woga na kutokuwa muwazi.
Inawezekana kuna mambo mengi ulidanganya ili uonekane wewe ni mtu Fulani lakini kadiri muda unavyokwenda unaona mateso unayopitia. Inawezekana ni watu uliowaahidi kuwafanyia mambo Fulani na hadi sasa umeshindwa kutekeleza. Inawezekana umekuwa mtumwa sana kwa kupitia mambo ambayo ulidanganya huko nyuma na sasa yanakutesa kwenye ndoa yako au mahusiano uliyonayo. Kama wewe umekuwa mtumwa suluhisho la utumwa ni uhuru.
Kuna watu wanaishi Maisha ya kuigiza naya mateso makubwa kwasababu ya uongo waliousema kipindi cha nyuma. Inawezekana ulidanganya jina lako ukapata cheti feki na sasa unatumia jina la mtu nah ii imekuumiza sana hasa unapolikumbuka jina lako. Ni wakati umefika wa kutoka kwenye kifungo hicho.
Yapo mambo mawili yanayowafanya watu waingie kwenye vifungo na kushindwa kutoka.
Kusema Uongo.
Inawezekana umedanganya sana na ili uonekane ulisema ukweli inakubidi ufanye mambo Fulani ya kuonyesha kwamba ulikuwa mkweli. Mambo hayo yanaweza kuwa mateso makubwa kwenye Maisha yako hivyo kukunyima uhuru wako.
Dawa ya kuondoka kwenye kifungo hiki ni kusema ukweli pekee yake. Hakuna namna nyingine ambayo unaweza kutoka kwenyen kifungo hiki kama hutosema ukweli. Amua kukataa Maisha ambayo unaishi ya kudanganya watu ili uridhishe mioyo yao na huku ukiteseka ndani ya moyo wako.
Kushindwa kusema Hapana.
Watu wengi wameingia katika mtego huu na wanateseka Maisha yao yote. Kuna waliongia kwenye mahusiano kwa shingo upande na sasa wanajutia maamuzi yao. Kwasababu tu mtu alikuwa yupo peke yake (single) akaamua tu akubali lakini hakuwa na upendo wa dhati. Baadae hali hii inaleta maumivu ya ndani. Huwezi kumuacha mtu huyu kwasababu utamuumiza lakini wewe unaendelea kuumia Zaidi ndani ya moyo wako.
Inawezekana umeingia kwenye mikataba ambayo huitaki kwa kulazimishwa na ukashindwa kukataa kutoka imekua ngumu kwako na hivyo umekuwa kifungoni.
Uhuru unakuja pale utakapoamua kuweka mambo yote wazi yanayohusika kwenye kukufanya uwe mfungwa. Amua sasa kuachana na mambo yote yanayokufanya ukose Amani ya moyo. Kama unaishi Maisha ya wasiwasi kwenye dunia hii kwasababu ya maamuzi uliyofanya bila kupenda ni wakati wako sasa kufanya maamuzi upya.
Leo nataka nikuonyeshe mahali ambapo unaweza kuupata uhuru wako tena. Uhuru wako upo kwenye kusema ukweli.
Kuna neno kwenye Biblia linasema “MTAIFAHAMU KWELI NAYO ITAWAWEKA HURU” Kweli pekee ndio ina uwezo wa kukutoa kwenye kifungo ulichopo.
Amua leo kuendelea na Maisha ambayo hayakuletei Amani ya moyo uanze upya Maisha ya uhuru.
Waambie ukweli ili utoke kwenye kifungo ulichonacho. Hakuna namna nyingine yaw ewe kuondoka kwenye vifungo hivyo ni kwa kusema kweli pekee.

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/kocha

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading