Kitu ambacho kila mmoja anakipigania ni Maisha bora.  Na maisha bora ni pale unapopata kile unachokitaka pamoja na kufurahia Maisha yako kwa ujumla na kile unachokifanya. Tukiweza kuujenga msingi bora wa Maisha yetu hatuwezi hata siku moja kujutia aina ya Maisha tunayoishi. Zipo sehemu mbili za muhimu sana kama utaweza kujenga msingi wako hapo Maisha yako yatakuwa ni bora sana.
Kwanini Upo Hai leo?
Hili ni swali ambalo kila binadamu anatakiwa awe anajiuliza mara kwa mara kwasababu linatuwezesha kurudi kwenye kulijua kusudi letu. Kitu cha kwanza ambacho wewe kama binadamu unatakiwa utambue sababu ya wewe kuwepo hai sasa.
Ukitambua upo hai kwa majusudi gani utaweza kuishi Maisha yenye manufaa kwasababu utakuwa unatimiza kusudi la kuwepo kwako. Ni hatari sana mtu kuishi Maisha ya bahati yaani hajui kwanini yupo duniani anafanya kila kinachomjia mbele yake. Kwenye kitabu cha Siri 7 za Kuwa hai Leo nimeelezea vyema kwanini Upo hai leo na sio jana, sio kipindi kingine chochote. Kwanini upo hai kama mwanadamu na sio kama mnyama mwingine. Ukiweza kutambua unaanza hatua nzuri sana ya kuwa na Maisha bora.
Unawezaje Kugusa Maisha ya wengine.
Ukitambua kusudi la kuwepo hai unaanza sasa kuangalia ni kwa namna gani kusudi hilo litagusa Maisha ya wengine. Yaani chochote Mungu alichoweka ndani yako sio kwa ajili yako ni kwa ajili ya wengine. Ukitaka kupata chochote unachokitaka unatakiwa utumie kile kilichopo ndani yako kuwapa wengine na watakuwezesha kupata chochote unachokitaka kwenye dunia hii.
Furaha ya kweli ipo kwenye kuyagusa Maisha ya wengine. Hakuna furaha kubwa kama kusikia kuna binadamu wengine Maisha yao yamekuwa bora kwasababu ya uwepo wako hapa duniani.
Na hakuna majuto makubwa kama kusikia kuna watu wanashindwa kupiga hatua kwasababu yako. Huwezi kuwa na furaha kama unawakwamisha wengine.
Maisha yako yatakuwa bora kama utaweza kugusa Maisha ya wengi Zaidi. Endelea kujiboresha ili utoe kilicho bora na Maisha yako hayatakuwa kama yalivyokuwa.
Usiache kusoma kitabu cha Siri 7 za kuwa Hai Leo kwani nimezielezea point hizi kwa kina Zaidi. Kitabu hiki inapatikana kwa mfumo wa Hardcopy na SoftCopy chukua mawasiliano yangu ujue namna ya kukipata.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Chukua Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading