Mambo mabaya yote yanayotokea kwenye Maisha yako sio kwa bahati mbaya kuna mahali uliyasababisha yakatokea. Badala ya wewe kuchukua muda mwingi kulaumu na kulalamika jiangalie kwa upande wako unahusikaje kusababisha.

Tuchukue mfano rahisi watu wawili wanagombana hadi kutaka kupigana, ukikaa na mmoja wapo ukamuuliza ilikuaje ataanza kumtupia lawama mwenzake. Lakini ukweli hadi wakafikia kugombana yeye pia kuna mahali alisababisha. Labda alitakiwa akae kimya tu asijibu lakini akajibu vibaya tena kwa hasira.
Tuje kwenye mahusiano, unaweza kufikiri mwenzako anakufikiria na kuhisi vibaya kwenye mambo unayoyafanya lakini pia kuna mahali umesababisha. Haiwezekani tu ikatokea mwenzako akaanza kuhisi wewe sio mwaminifu kuna vitu ulifanya ambavyo vikawa vinampa wasiwasi. Sasa ukikaa na huyu anaelalamika kufuatiliwa sana ataanza kukwambia “ooh mwenzangu ana wivu sana”. Lakini ukweli kuna mahali alisababisha mwenzake akaanza kupata wivu juu yake.
Sasa ni vyema sana wewe binafsi kabla hujaanza kutupa lawama kwa mwenzako au kwa jambo unalopitia embu hakikisha umejiangalia mwenyewe ni kwa namna gani umesababisha mambo hayo yakatokea. Labda ulikua mzembe, ulikosa uaminifu, ulifanya mambo yanayotia wasiwasi. Na mengine mengi. Usiwe mwepesi wa kutupia wengine lawama juu ya matatizo yanayotokea kwako kwasababu pia haibadilishi tatizo wala haileti suluhisho lolote. Jirekebishe na uache mambo yoote yanayoweza kufanya uonekana wewe sio mwaminifu au kukosea mara kwa mara.
Ni uhakika kabisa embu kaa chini leo jitazame na ujiulize mambo yale unayoona wengine ndio wanahusika wewe umehusika vipi kufanya yatokee. Umeachwa na wapenzi mara nyingi badala ya kulaumu na kusema wamekuchezea embu jitazame wewe ulisababisha vipi. Labda uliwaamini sana, labda una tabia ambazo wenyewe waliziona kwamba hazifai kuendelea na wewe, labda kuna mahali ulikosea haiwezekani ukapatwa na matatizo wewe halafu asilimia mia moja wahusika wawe wengine.
KUMBUKA: KUNA MAHALI ULISABABISHA. Na ukishagundua hivyo usibakie hapo embu badilika basi. Ukishajua wewe kuna uzembe unafanyaga mahali ndio maana unaachwa embu badilika. Ukishajua kuna matendo yako Fulani yanasababisha mwenzako apate wasiwasi na wewe embu yaache maana hapo ndio utakuwa umetatua tatizo.
#USIISHIE NJIANI
Usiache kusoma Kitabu cha Siri 7 za kuwa hai leo wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading