Kujisemesha mwenyewe ni njia nzuri sana ambayo unaweza kuitumia kutengeneza siku ambayo ni bora sana. Vile vile kwa kujisemesha mwenyewe kutakuasaidia USIISHIE NJIANI kwenye lile jambo uliloamua kulifanyia kazi. KUJISEMESHA MWENYEWE ni tiba ya akili na moyo wako hasa pale unapokuwa umeanza kupitia magumu katika kuitimiza ndoto yako.

Unapopitia hali mbaya labda ni hasara kwenye biashara, umesemwa vibaya na watu njia pekee ya kuweza kutengeneza picha chanya kwenye akili yako ni KUJISEMESHA MWENYEWE vile vitu ambavyo ndio unataka vitokee kwenye Maisha yako.


Kama wewe ni masikini basi usiseme nitakuwa tajiri jisemeshe kwa kusema MIMI NI TAJIRI. Sema kile unachokitaka kwa wakati uliopo na sio wakati ujao. Jisemeshe kana kwamba ni tayari umeshapata kile unachokitaka.
Ukitaka kuwa na siku bora unapoamka asubuhi jisemeshe vile unavyotaka vitokee siku hiyo. Kama wewe ni mfanya biashara embu jisemeshe kwa kutaja idadi ya mauzo unayotaka kwenda kuuza siku ya leo. Taja idadi ya wateja unaotaka waje kwenye biashara yako leo.
UNAPOJISEMESHA MWENYEWE yale maneno unayotamka yanaingia katika ubongo wako wa ndani ambao ndio unasababisha matokeo. Hivyo hata kama umechoka usiseme nimechoka sema nina nguvu. Kama unaumwa usisme najisikia vibaya sema mimi ni mzima kabisa.
Mimi ni Tajiri.
Ninaendesha Gari ya ndoto yangu (litaje)
Ninamiliki Pesa (Taja Kiasi).
Ninakwenda kuwa na siku bora yenye mafanikio.
Ninatengeneza Kipato (kitaje) Kila siku.
Ninakwenda kuuza (taja Unachouza na Kiasi Unachotaka kuuza Leo)
KUJISEMESHA MWENYEWE ni harakati ambazo zimeanzishwa na rafiki yangu Zingo The Great. Nampa pongezi sana. Kwa kupitia kujisemesha mwenyewe unaweza kutimiza kile unachokitaka.
#USIISHIE NJIANI
Usiache kusoma Kitabu cha SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading