HATUA YA 211: Hakuna Tena Wa Kukuchapa.

jacobmushi
1 Min Read
Ulipokuwa mdogo kuna mambo ulikuwa ukifanya kinachokuja kufuata ni viboko.
Mfano ukikutwa umepanda juu ya mti,  umegusa vitu ambavyo uliambiwa usiguse. Na mengine mengi unayokumbuka.

Sasa wakati huu umekuwa mtu mzima usikubali kuendelea kuwa na mtazamo ule ule wa kitoto wa kuogopa watu.  Unajua Ulipokuwa mtoto ungeachwa bila ya kuchapwa inawezekana ungegunduaga mambo mengi sana. Lakini kwasababu ulionekana kama mharibifu fulani hivi usiejua kitu hivyo ukaishia kula viboko.

Kinachonishangaza sana ni watu wazima wa kipindi hiki bado wanaogopa wazazi  na watu wanaowatazama kama vile watachapwa.
Ukweli ni kwamba ukianza biashara labda ukapata hasara hakuna wa kukuchapa. Zaidi unapata kiti cha kujifunza.

Wewe una kipaji kizuri sana ndani yako hadi leo unaogopa kusimama na kukionyesha kisa tu unaogopa sijui huna nini,  sijui hujasoma,  sijui huna watu wa kukusaidia. Embu achana na hayo mawazo.

Hakuna tena aliekuandalia fimbo eti ukifeli maisha aje akuchape. Kama umeamua kufanya fanya usiwaangalie watu.

Usiwaangalie unaowahofia,  waangalia wanaokukubali na wanaokushangilia. Ukishapata ushindi ndipo geuza macho uwatazame wale ulikuwa unawaogopa

USIOGOPE SONGAMBELE  HAKUNA TENA WA KUKUCHAPA.

#USIISHIE NJIANI

Usiache kusoma Kitabu cha Siri 7 za kuwa hai leo wasiliana nami kwa 0654726668.

Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading