Huu msemo umekuwa maarufu sana kipindi hiki. Leo nataka nikuambie kwanini upambane na hali yako. kama ulikuwa hujui basi ni muhimu sana ukafahamu kwamba unatakiwa upambane na hali yako.

 

Chochote kinachoendelea kwenye Maisha yako unapaswa kupambana nacho kukibadilisha. Hakuna mtu mwingine anahusika na hali unayopitia kwa saa n ahata tangu zamani. Labda kama wewe ni mtoto mdogo au mzee asiyejiweza. Kinyume nah apo lazima upambane na hali unayopitia.
Hakuna mtu mwingine anaifikiria hali unayopitia iwe mbaya au nzuri hivyo ni muhimu sana ukapambana kuibadilisha.
Hakuna mtu mwingine anaejua uhalisia wa ugumu wa Maisha yako hata kama utamwelezea vizuri bado hawezi kuona ugumu kama wewe unaoupitia.
Kama unachukia hapo ulipo unachotakiwa kufanya ni kuondoka hapo sio kutoa sababu yeyote ile. Pambana na hali yako kwa kweli, usipotoa jasho hakuna kitakacho badilika.
 Hivyo basi usichukie hata kidogo mtu anapokwambia pambana na hali yako anamaanisha kweli upambane nayo. Anamaanisha ubebe majukumu yako vizuri. Hakuna mtu mwingine anahusika na majukumu yako ya Maisha.
Hivi unajua kuna mambo usipoyapa kipaumbele kwenye Maisha yako hakuna mtu mwingine atakuja kukusaidia kufanya hivyo? Mfano una njaa usipoamua kwenda kula hakuna mtu mwingine atakuja akwambie nenda kale lazima uamue kutoka ndani yako.
Hata mimi nakwambia tambua majukumu yako ni yapi kisha UPAMBANE NA HALI YAKO.

 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading