Kutazama tazama nyuma kumekuwa sababu ya wengi kugeuka na kurudi walipotoka. Wakati changamoto zimekuwa nyingi kwenye safari yako ndio wakati hasa wa kutazama mbele badala ya kule ulipotoka.

Wakati kuna giza ndio wakati hasa wa kutafuta mwangaza. Wakati tumefika sehemu hatuoni njia ndio wakati wa kutafuta njia.

Kinachowafanya wengi washindwe kufika popote ni kwasababu hakuna jambo lolote ambalo wamejitoa kikamilifu kulifanya hadi liwaletee matokeo wanayotaka.

Umeamua kuingia kwenye mahusiano jitoe kikamilifu usiingie nusu nusu. Acha vyote ambavyo vinaweza kuwa sababu ya wewe kurudi nyuma tena. Kaa mbali na vishawishi ambavyo vinaweza kuwa sababu ya wewe kupunguza upendo. Haijalishi unapitia changamoto gani kama ni kweli umejitoa hutaangalia nyuma bali utatafuta njia ya kusonga mbele.

 

Kitendo cha wewe kutazama nyuma ni kujiletea vishawishi vya kukwambia kwamba ulikosea kufanya uchaguzi. Kutazama nyuma kutakufanya uanze kuona uzuri wa kule ulipotoka na kutamani tena ungekuwepo kule.

Kilichowafanya wana wa Israel wakashindwa kumaliza safari yao ya kwenda Kaanani na wakafia jangwani sio ugumu wa safari au hali ngumu ya jangwani bali ni kitendo cha wao kutazama Misri na kumlalamikia Musa. Kitakachokufanya wewe upoteze hayo mahusiano uliyonayo sasa hivi sio ugumu wa mahusiano bali ni wewe kutaka kufananisha kule ulipokuwa na hapo ulipo sasa hivi.

Umeingia kwenye biashara ingia moja kwa moja kama utakuwa mtu anaetazama urahisi uko wapi utaishia kushindwa na kurudi nyuma.

Haijalishi wateja watakosekana au ugumu utatokea wapi kitakachokufanya uache au uendelee ni kiwango ulichojitoa kwa ajili ya biashara yako.

Hakuna tatizo lisilo na suluhisho na kama umefikia sehemu ukaona hakuna suluhisho tena basi ujue hilo sio tatizo.

Kama umeamua kwenda nenda acha kukumbuka mambo mazuri ya zamani yatakuwa sababu ya wewe kushindwa kuendelea mbele Zaidi.

 

Kama uliamua kuondoka nyumbani ambapo kulikuwa na kila kitu ambacho ungehitaji ukaingia kwenye maisha ya kujitegemea halafu ugumu ukaanza kuuona ukijikuta unakumbuka maisha yalivyokuwa mazuri nyumbani. Unapata kila unachokitaka, ukiomba pesa unapewa haraka sana, ukiendelea kukumbuka sana siku si nyingi utafungasha urudi nyumbani.

 

Umemua kuishi na mtu hali inakuwa ngumu badala ya kutafuta suluhisho unaanza kusema “nilipokuwa nyumbani hakuna nilichokuwa nakosa” sasa unasahau kuwa hapo sio nyumbani kwenu hapo ni kwako. Kama umeamua kufanya jambo acha kukumbuka kule ulipotoka hasa wakati unapitia magumu.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading