Mara nyingi tumekuwa tunapambana na mambo ambayo hayaondoi matatizo yetu bali yanayapooza tu na kisha baada ya muda hujirudia.  Kama kuna sehemu inavuja kwenye nyumba yako suluhisho sio kukinga maji yanayodondoka bali ni kuziba pale panapodondosha maji.

Watu wengi tumekuwa tunatatua matatizo yetu kwa mfumo huu wa kutega ndoo kukinga maji yanayovuja badala ya kuziba tundu linalotoa maji.

Kama mti unatoa matunda mabovu hupaswi kuhangaika na matunda bali mizizi ya mti. Ukiona hakuna mabadiliko unang’oa kabisa mti unapanda mwingine.

Maisha yako yataendelea kuwa magumu kama utaendelea kupambana na matokeo badala ya chanzo cha matokeo. Kama umekuwa na madeni mwaka 2017, hayo ni matokeo ya kutokuwa na nidhamu ya fedha.

 

Kama umekuwa unafanya mambo na hayatokei embu nenda kwenye chanzo cha hayo unayotaka kufanya. Chanzo kinaweza kuwa ni wewe mwenyewe hivyo shughulika na wewe badala ya kushughulika na mambo yaliyotokea au yanayokwama.

Kama umetapeliwa rudi kwenye chanzo kwanini umeingia kwenye mtego wa utapeli? Fukua chanzo utagundua kuna sehemu ya kurekebisha ila ulete matokeo mazuri.

 

Haiwezekani hata siku moja mti wa limao ukazaa machungwa, hivyo matokeo unayopata yanadhihirisha wewe ni mtu wa namna gani.

Ukitaka kubadilisha chochote kwenye Maisha yako kinachokwenda vibaya nenda kwenye chanzo chake. Ukitaka kuondoa tabia yeyote ambayo inakuletea matokeo mabovu Maishani mwako ondoa mizizi yake usije kukata shina peke yake ipo siku mti utachipuka tena.

 

Hakuna jambo lisilo na chanzo, ukiweza kushughulikia chanzo unaweza kumaliza tatizo linalokusumbua maishani mwako.

Maisha yako ni mkusanyiko wa matukio madogo madogo yanayotokea kila siku, kama kuna tukio unataka kubadilisha rudi mwanzo kabisa angalia ni chanzo kipi kinaleta matokeo unayopata?

Ukitaka kubadili anza na chanzo.

 

” Kama umependa Makala Hii Usiache Kuweka Maoni yako Hapa chini”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,

Simu: 0654 726 668,

Twitter: jacobmushitz

Instagram: jacobmushi

Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Barua pepe: jacob@usiishienjiani.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading