HATUA YA 321: Ukichukua Hatua ya Imani, Utaanza Kuona Usiyoyatarajia.

Kuna Mambo hutakaa uyaone kwenye Maisha yako hadi uamue kuchukua Hatua ya Imani. Hatua ya Imani ni kutoka na bidhaa zako nyumbani kwenda nazo mtaani ukiwa hujui nani atakwenda kuzinunua na ndio mara ya kwanza.

Hatua ya Imani ni kuanza kufanya lile wazo ulilokuwa unaogopa sana watu watasemaje au watanionaje. Kuna baraka zitaanza kufunguka kwenye Maisha yako unapoanza kuchukua Hatua ya Imani.

Kuna mengi utaanza kujua kuwa yanawezekana pale tu utakapoanza kuchukua Hatua. Imani yako ndio itafungua milango ya vitu ambavyo vilifungwa.

Hakuna mtu atakaejitolea kuja kukusaidia kama hajaiona juhudi yako yeyote ya kutaka kutoka hapo ulipo. Hatua ya wewe kutaka kuinuka ndio itavuta watu waje kukuunga mkono.

Jitazame una nini?

Unaweza nini?

Una ujuzi gani?

Kitu gani unaweza kufanya kikawa msaada kwa wengine?

Anzia hapo hapo usitake kuanza na Hatua ya 100 anza na Hatua ya kwanza. Hata kama ni kufagia anza kwa kufagia hadi utoke kwenye kufagia ufike viwango vya juu.

Wengi wanapenda kuanza kitu ambacho kila mtu atakikubali, biashara ambayo kila mtu akiona atavutiwa nayo. Ukija kwenye mifuko yao hawana chochote. Sasa kwanini usikubali kuanza na kile kidogo ambacho wewe unafikiri hakitoshi?

Kwanini usikubali kuanza kumhudumia mteja mmoja hadi wateja  kumi? Anzia hapo ulipo ukipata faida ndogo ambayo umeifanyia kazi kweli itakupa hamasa ya kusonga mbele Zaidi.

Nenda kachukue Hatua ya Imani. Anza hapo ulipo, fanya kile ulichokuwa unakiogopa sana.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *