HATUA YA 328: Hii Ndio Sababu ya Kushindwa Mambo Magumu.

Mara nyingi unapoamua kufanya jambo la tofauti na lenye ugumu tofauti na ulivyozoea kunakuwa na hofu ndani yako. Hofu ya kushindwa,hofu ya kupata aibu, hofu ya kusemwa na za aina nyingi. Pamoja na hofu mbalimbali ambazo zitakuwa ndani yako bado unakuwa na nafasi ya kupata matokeo bora endapo tu mtazamo wako kwenye hilo jambo utakuwa sahihi.

Mtazamo wako unapokuwa mbaya yaani ukajijengea mtazamo wa kushindwa ni lazima utapata matokeo ya kushindwa. Kinachoamua matokeo sio hofu zinazoletwa na watu bali ni mtazamo ulioujenga wewe mwenyewe.

“It is our attitude at the beginning of a difficult task which, more than anything else, will affect its successful outcome.” -William James

William James anasema ni mtazamo wetu pale tunapoanza jambo gumu ndio unasababisha matokeo kuliko kitu kingine chochote. Endapo utaweka mtazamo sahihi basi utaweza kuzishinda hofu. Utaweza kuyashinda maneno ya watu. Utaweza kuzshinda changamoto zozote zitakazotokea mbele yako.

Kuwa na mtazamo sahihi haimaniishi hutapata changamoto, bado changamoto zitakuja ila utaweza kuzivuka kwasababu umejiwekea mtazamo wa kushinda. Anza kujiona wewe ni mshindi kwenye kila unachokwenda kukifanya. Anza kuona matokeo chanya.

Endapo utakuwa na mtazamo chanya na bado yakaja matokeo tofauti na ulivyotarajia bado usikate tamaa na kuanza kubadili mtazamo wako. Kwani ukibadili mtazamo ndio utakuwa umekaribisha kushindwa.

Mtazamo wako kwenye kila jambo ndio unaamua matokeo.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

https://jacobmushi.com/patavitabu/

This entry was posted in HATUA ZA MAFANIKIO on by .

About jacobmushi

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *