HATUA YA 383: Ni Haki Yako Lakini Lazima Uumie

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Unajua kila kitu kizuri hapa duniani ni kwa ajili ya kila binadamu? Unajua kwamba hata wewe unastahili dhahabu, ndege, au chochote kizuri? Unajua kila ambacho umekuwa unakitamani kwenye akili yako ni sawa kabisa?

Ni kweli ni haki yako, mafanikio ni haki yako, utajiri ni haki yako, kuwa mtu mkuu ni haki yako. Lakini  sasa ili uvipate vyote hivyo lazima uumie sana. Hakuna mtoto anaerithishwa ufalme kama anaoenakana ni mzembe mzembe lazima atapitia mafunzo mbalimbali ili akomae.

Kuna vitu ili viweze kudumu katika mikono yako lazima kwanza wewe uumie vya kutosha. Lazima utoe gharama ya kupata. Kama hujakomaa ni ngumu sana kudumu kwa vile vitu ambavyo ni haki yako.

Kwenye biblia kuna mfano wa mwana mpotevu na baba yake Tajiri. Yule mtoto alilia haki yake akapewa lakini kwasababu alikuwa hajakomaa akaenda kupata maumivu ambayo yalimpa akili za Maisha. Hata wewe ikitokea umepata chochote bila ya kuumia na kupata ukomavu utavipoteza.

Ufalme ni haki yako lakini mpaka uondokane na utoto kwanza ndipo uweze kuruthishwa ufalme. Rafiki yangu nafurahi kuona unasoma Makala hizi maana hizi ndio mojawapo ya gharama unazopaswa kulipa ili uweze kumiliki vitu vikubwa.

Lazima ukubali kununua Vitabu usome, kulipia semina za gharama kubwa kubwa ili uweze kukutana na watu ambao wamefika viwango vya juu wakubebe Zaidi. Unajua kuna watu hutaweza kukutana nao kama utaendelea kubakia kwenye Hatua hiyo ambayo upo sasa. Lazima ukubali kufanya kitu cha ziada ili uweze kwenda Hatua ya ziada.

Rafiki mafanikio ni haki yako lakini ni lazima ukubali kuumia. Kuishi ni haki yako lakini lazima ujitafutie Maisha bora ili uweze kufurahia kuishi.

Nikutakie kila la Kheri,

 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading