Kwa kawaida Akili ya mwanadamu muda wa asubuhi inakuwa na nguvu sana na uwezo mkubwa wa kufikiri. Kama una kazi ngumu ukizianza asubuhi unajikuta umeweza kuzimaliza kwa haraka sana.

Kwa kawaida unashauriwa wakati wa asubuhi ndio mzuri kufanya zile kazi ambazo ni nzito au zinazochosha akili yako. Hii itakuwezesha wewe baadae ukiwa umechoka umalizie na kazi nyepesi kabisa na siku yako iwe imekwenda vyema.

Vilevile tulipokuwa shuleni kipindi cha Hesabu au masomo mengine magumu mara nyingi asubuhi ndio vinapewa vipaumbele kwasababu ndio wakati ambao akili inakuwa haijaingiza vitu vingi.

Kitu cha ajabu sana ambacho wengi tunacho na tumekuwa tunaiga kwa wengine au basi tumeona ni utaratibu wa maisha yetu kila siku, na bila kujua kumbe tunajiharibia siku zetu. Unapoamka asubuhi ukaanza siku yako kwa habari unaharibu siku yako kabisa.

Hii ni kwasababu vyombo vingi vya habari huzipa vipaumbele taarifa hasi ili kuvutia watazamaji na wasikilizaji. Ubaya wa taarifa hasi unakuja pale ambapo unainza siku yako ukiwa umechoka na kuona kama dunia ipo kwenye hali mbaya sana.

Mimi binafsi kuna kipindi nilikuwa nafuatilia taarifa hadi nikaanza kuona kama kuna hali mbaya ya hatari sana inakuja kutokea siku za karibuni. Lakini hadi sasa sijawahi kuiona hiyo hali mbaya. Ukizipa kipaumbele habari unaharibu siku yako.


Ni bora asubuhi yako uijaze maarifa bora ambayo yatakusaidia kwenye shughuli zako za kila siku. Sio lazima ujue kila linaloendelea hapa nchini au hapa duniani. Labda tu liwe na umuhimu Fulani kwenye maisha yako.
Kuna hali mbaya zinatokea kwenye maisha yako sio kwasababu ya hali ya dunia nzima bali kwasababu ya taarifa ulizojaza kichwani mwako.

Ukiamka asubuhi tafuta Kitabu kizuri cha Sauti ambacho kinaweza kukuhamasisha au soma kitabu kizuri cha kukufungua akili. Vile vile kama unatembelea mtandao huu kila siku asubuhi utakutana na Makala nzuri ya kukufanya upige hatua kwenye maisha yako.


Siri 7 za Kuwa Hai Leo Kitakuwa mikononi mwako Hivi Punde Kaa Tayari weka oda yako kwa namba 0654726668.

Karibu Sana.
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading