Hamasa ndio chanzo cha matendo ya aina zote unayoyaona duniani yakifanyika. Kama huna hamasa unashindwa kufanya jambo kwa ufanisi
Ukifahamu kinacholeta hamasa ndani yako unaweza kujihamasisha na ukatimiza ndoto na malengo yako. Zipo njia mbalimbali ambazo unaweza kuzitumia kama chanzo cha kuinua hamasa yako ili ufanye jambo                 Njia mojawapo ni kuzungumza maneno chanya ndani yako kuhusu wewe.
Zipo aina mbili za Hamasa
Hamasa ya Nje
Hamasa ya ndani
Hamasa ya Nje           
Hamasa ya nje ni kama, pesa, kukubalika kwenye jamii, umaarufu au hofu.
Hamasa inayoletwa na hofu.
Hofu ya kupata aibu inaweza kukufanya upambane na ukafanikiwa. Hofu ya kuachwa kwasababu huna pesa inaweza kukufanya ufanye kazi hadi ufikie ndoto zako. Hofu ya kufukuzwa kazi inaweza kukufanya ufanye kazi kwa bidii. Hofu ya kesho itakuaje inaweza kuwa sababu ya wewe kuchukua hatua leo na ukaweza kubadili kitu kwenye maisha yako.
Ukiwa umeajiriwa ukapangiwa majukumu na bosi, akasema anakuja kukagua muda fulani. Kwasababu ya hofu ya bosi unaweza kufanya kazi kwa wakati muafaka na ukaifanya vizuri sana.
Kilichokufanya ukachukua maamuzi hayo bila kujali kuumia au ule umbali ni hamasa inayoletwa na hofu ya kung’atwa na nyoka.                      Hasara za Hamasa hii ni kwamba, inakuwepo mara moja tu na hupotea haraka.
Baada ya kupata pesa kidogo utaridhika na kusahau kuwa safari inaendelea. Baada ya kutatua tatizo utaendelea na maisha yako ya kawaida.
Hamasa ya Motisha                       
Hamasa ya Motisha ni kama unapopandishwa cheo, unaongezewa mshahara. Unapopewa Zawadi, pongezi. Hamasa hii inawafanya watu waongeze bidii kwenye nafasi zao. Shuleni ukifanya vizuri unatanywa ili kukuhamasisha wewe na wengine pia. Unapewa Zawadi ili uendelee kufanya vizuri zaidi. Unaongezewa mshahara ili uongeze uzalishaji kwenye nafasi yako.
Hasara za hamasa hii ni kwamba inaisha pale unaporidhika na kile ulichopewa. Ukimpandisha mtu cheo ukampatia gari, nyumba, mshahara wa kutosha baada ya muda ataanza kuridhika na yale alopata na kazi itakuwa mbovu, na wakati mwingine uzalishaji kushuka.
Hamasa ya pili ni Hamasa inayotoka Ndani                       
Hii ndio hamasa unayoihitaji zaidi kuliko hamasa nyingine zote.                     Hamasa ya ndani ndio inatuwezesha tutimize ndoto zetu.                       Ukikosa hamasa hii huwezi kwenda popote. Hamasa hii inaletwa na.yale majukumu uliyonayo kila siku. Majukumu ya kutimiza kusudi lililopo ndani yako. Hamasa hii inajengwa kwa kuzitizama ndoto na malengo yako kila siku.
Unatakiwa uwe unayasoma.mara kwa mara. Jineneee vile unavyotaka uwe. Jijengee picha kubwa ya maisha yako na iseme.mara kwa mara                        Jihamasishe mwenyewe, hamasa inayotoka ndani huwa haiishi ila inaweza kushuka tu. Hamasa itokayo ndani haipotei kwasababu wewe mwenyewe ndio.unajipatia
Mambo yanayokufanya upoteze hamasa.  
                     
Kukosolewa kusiko sawa.
Hapa ni pale mtu anapokukosoa kwa makusudi tu. Kwenye jambo unalolifanya ili usiendelee.
Kudhalilishwa Mbele za watu                       
Hii inaweza kutokea kazini, au shuleni au popote pale na inahusika sana katika kuua vitu vilivyopo ndani ndani ya wengi. Mtu anaweza kufanya kwa makusudi au bila kukusudia.
Kuwapongeza wasio stahili na kuwaacha waliostahili. Kushindwa pia ni chanzo cha kushusha hamasa. Kukosa mwelekeo wa maisha ni sababu ya kupoteza hamasa yako. Kukosa malengo ni sababu ya kupoteza hamasa yako
Kukosa vipaumbele  
                     
Kujizungumzia maneno mabaya.
Mfano:
Mimi ni mdogo sana.
Kwetu ni maskini
Nimefeli shule
Nina sura mbaya
Nina sauti mbaya
Yaogope maneno unayosema juu yako kwani yanajenga na kubomoa
                     

 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading