Connect with us

HATUA YA 80: Washangaze kwa Vitendo..

HATUA ZA MAFANIKIO

HATUA YA 80: Washangaze kwa Vitendo..

Wako wengi sana walipokuona unaanza walikukatisha tamaa na kusema kwamba hutaweza jawabu sio kurudi nyuma. Unatakiwa uwashangaze, waonyeshe kuwa umedhamiria kabisa kufanya hicho unachokifanya hadi ufikie mafanikio. Washangaze kwa kasi yako ya kusonga mbele, unajua hawaamini walikuwa wanakuona wewe ni mtu wa kawaida sasa ukirudi nyuma ndio watakuwa wamejithibitishia kwamba wewe ni wa kawaida. Washangaze […]

Wako wengi sana walipokuona unaanza walikukatisha tamaa na kusema kwamba hutaweza jawabu sio kurudi nyuma. Unatakiwa uwashangaze, waonyeshe kuwa umedhamiria kabisa kufanya hicho unachokifanya hadi ufikie mafanikio.

Washangaze kwa kasi yako ya kusonga mbele, unajua hawaamini walikuwa wanakuona wewe ni mtu wa kawaida sasa ukirudi nyuma ndio watakuwa wamejithibitishia kwamba wewe ni wa kawaida.

Washangaze kwa kuweka matendo sio maneno washangaze kwa matokeo unayoyapata. Washangaze kwa mabadiliko kwenye Maisha yako. Hakuna kitu kikubwa kinachowafanya watu waanze kukuamini kama matokeo ya kile ulichokuwa unakisema mbele yao.

Hakuna namna nyingine ya kuwathibitishia kwamba wewe una weza bila ya kuweka vitendo na vitendo vikakuletea matokeo.

Labda walidhani kwakuwa umefeli na huna elimu ya kutosha basi utashindwa kwenye biashara uliyoianza. Ni wakati wako wa kuwashangaza ongeza bidi hadi uweze kuajiri hata wale waliosoma Zaidi yako.

Maneno machache vitendo vingi ndio matokeo ya kweli huonekana. Usipoteze muda mwingi wa kuwaelesha kwa mdomo wa kuelewe tumia muda huo kufanya kwa vitendo hadi upate matokeo. Matokeo ndio majibu ya maswali yao.


Kumbuka haufanyi hivyo kwa nia ya kuwaonyesha watu bali kwa ajili ya kutimiza maono yako. Katika kufanya hivyo majibu ya maswali yao yatakuwa yamejibiwa.

Huwa tunatumia nguvu nyingi sana kuwaelewesha watu kwa maneno laiti tungeweka nguvu ile kwenye matendo tungekuwa mbali sana. Majibu ya maswali yao yangejibiwa moja kwa moja.

Karibu sana.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
Email: jacob@jacobmushi.com
Blogs: www.jacobmushi.com

jacobmushi.com
Continue Reading
You may also like...

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in HATUA ZA MAFANIKIO

To Top