Tabia ya Uvivu ndio inasababisha wengi wanapata hasara ya maisha pamoja na matatizo mbalimbali.
Tabia ya Uvivu mara nyingi huletwa na kuridhika na kile unachokipata.
Kama mtu ana uhakika wa kupokea laki nane kwa mwezi anajisahau kabisa kwamba hana umiliki na kazi yake. Badala ya kuongeza bidii na Kutafuta chanzo kingine cha mapato mtu huyu anaridhika kabisa.
Hali huja kuwa ngumu sana pale anapopoteza kazi yake na hajui pa kwenda. Tuseme wewe umefanya kazi miaka mitano mfululizo na ulikua unalipwa mshahara mzuri tu lakini ukajisahau ukidhani kazi utakuwa nayo milele. Badala ya kujiongeza na kuanzisha biashara nyingine pembeni ukategemea mshahara kwa 100% mwaka wa tano ukafukuzwa kazi. Embu nambie utakuwa kwenye hali ghani?
Ulikua unasoma sana vitabu wakati ule mambo yanapokuwa magumu pamoja na kuomba ushauri lakini tangu mambo yalipoanza kwenda poa umejisahau kabisa vitabu husomi, na wala huhudhurii mafundisho. Unategemea nini ukipata hasara kubwa?
Kama unadai upo bize nakuhakikishia kuna walioko bize kuliko wewe na wanasoma vitabu na kujifunza kila siku.
Kama kweli una mpango wa kufanya mabadiliko kwenye maisha yako mwaka 2017 acha mara moja tabia ya Uvivu. Anza kusoma vitabu jiwekee ratiba yako mwenyewe. Hudhuria semina na mafundisho. Tenga bajeti maalumu kwa ajili ya kununulia vitabu.
Wengine ni wavivu hata kubonyeza hii link ya blog ili wasome wanaona ngumu. Wanataka waletewe kila kitu mdomoni. Mafanikio hayaji kirahisi hivyo bila kulipa gharama.
Swali la Mwisho : Mwaka 2017 umejiandaaje Kusoma vitabu?
Karibu sana nikutakie Siku Njema.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
Email: jacob@jacobmushi.com
Blogs: www.jacobmushi.com, www.jacobmushi.com
jacobmushi.com
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
Email: jacob@jacobmushi.com
Blogs: www.jacobmushi.com, www.jacobmushi.com
jacobmushi.com