Watu wengi tumekuwa tunatamani sana kupiga hatua katika maisha yetu na kufikia mafanikio. Lakini kumekua na vitu mbalimbali vinaturudisha nyuma na kutuzuia.

Inawezekana mwaka huu uliweka malengo na mipango lakini haujakamilisha kwa kiwango kikubwa. Mwaka 2017 unaweza kufanana kabisa na mwaka huu au ukawa ni mwaka ambao utafungua milango kwenye maisha yako. Inategemea tu na wewe umeamua nini. Maamuzi unatakiwa uanze kuyafanya sasa amua leo kubaki hivyo ulivyo au amua kubadilika na maisha yako yabadilike.

Amua leo kuacha tabia zile zilizokuwa zinakurudisha nyuma au ubaki navyo na maisha yako yaendelee kuwa yalivyo. Maamuzi yote yapo mikononi mwako. Unaweza kuamua kusonga mbele au kurudi nyuma.

Tabia za matumizi mabaya ya pesa,  muda,  na kutokuchukua hatua zinaweza kukurudisha nyuma kabisa usipoziacha.

Nafasi unayo ni wewe kufanya maamuzi sasa ni kitu gani unakitaka.

Jiunge na Semina Itakayoanza Tarehe 2/1/2017 ambayo itakua ni mwongozo wako wa mafanikio katika mwaka 2017.

Karibu sana.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author.
Phone: 0654726668
Email: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading