475; Huu ndio Ukosoaji Ninaoupenda.

By | March 20, 2019

Mwanzoni simu za smartphone zilipoanza kuja kulikuwa na tatizo kubwa la simu hizo kutokukaa na chaji. Baada ya muda sio mrefu wakaja watu wakaleta Power Bank ambayo inahifadhi chaji.

Tatizo linguine likaanza kuonekana kwenye simu hizi ni vioo kupasuka mara kwa mara. Haichukua muda wakaja na Screen Protector. Yaani unanunua simu halafu unakuja tena unanunua na screen protector pembeni.

Inawezekana katika hayo matatizo mawili makubwa ya simu hizi watu wengi waliishia kulalamika na kukosoa matatizo hayo. Lakini ni watu wachache waliamua kufikiria na kuja na suluhisho. Nataka ujifunze kitu hapa, badala ya wewe kuwa mtu anaekosoa kila kitu embu jaribu kufikiri uje na ukosoaji wa aina hii.

Badala ya kuendelea kusema hizi bidhaa ni mbaya hawaweki kitu Fulani embu jaribu kufikiri unawezaje wewe kukiuza hicho kitu. Tumekuwa na watu wengi sana wanaokosoa kwa maneno badala ya vitendo, tungewapata wakosoaji wa vitendo hakuna mtu angegundua bidhaa bila kufikiri kwa kina juu ya kitu ambacho amekiacha nyuma.

Jitazame wewe tangu mwaka umeanza umekuwa mtu wa kulalamika mara ngapi? Umekosoa vitu vya wat umara ngapi? Huo muda wa kukosoa kwa maneno ungeweza kuja na ubunifu mkubwa ambao ungeleta mapinduzi ambayo wewe ungenufaika, wateja wangenufaika na huyo unaemkosoa angejifunza pia.

Acha sasa kuendelea kukosoa kwa maneno kama tuanze kukosoa kwa vitendo. Kama unaona mtu hafanyi vizuri kwenye kitu Fulani na huna uwezo wa kwenda kumuelekeza moja kwa moja, jaribu kufikiri ni kitu gani unaweza kugundua kilete manufaa kwa ile kero unayoiona.

Nakutakia kila la Kheri.

Rafiki Yako Jacob Mushi

www.jacobmushi.com

2 thoughts on “475; Huu ndio Ukosoaji Ninaoupenda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *