Maneno mengi uliyoambia tangu ukiwa mdogo kwamba hauwezi, haiwezekani kwenu ni maskini, kwenu wote hawajawahi kufaulu. Ukaonyeshwa hata na watu wako wa karibu kama wajomba mashangazi mama wadogo na wakubwa, kaka zako, waliojaribu wakashindwa huwezi kuyaondoa kwa siku moja. Maneno hayo yamejishika katika ufahamu wako hivyo wakati mwingine yanakurudisha nyuma.
Kuna wakati unapitia hali ngumu hadi unafikiria hivi ni kweli yale niliyoambiwa kua kwetu tuna laana eeh! Unajikuta una madeni kila kona hadi unahisi umeanza kua kama yule babu yako wa zamani uliehadithiwa habari zake. Umekua na magumu hadi unaona kama ndoto na malengo yako yataishia kwenye makaratasi tu.
Hata watu wako wa karibu wanaanza kukusema kwa kua yale uliyowaambia yatakwenda kutokea wala hawaoni dalili. Wengine wanakwambia achana na hizo story za mafanikio.
Leo nakwenda kukutia moyo kua ukiona giza linaongezeka ujua pamekaribia kukucha. Ukiona mateso yamezidi kua mengi tambua kua ni wakati wako wa kufunguliwa. Ukiona kila unachokifanya hakileti matokeo jua ndio unakikaribia kile cha uhakika. Jack Ma tajiri wa kichina aliwahi kusema haya;
Never give up. Today is hard, tomorrow will be worse, but the day after tomorrow will be sunshine. Jack Ma
 
Usikate tamaa leo ni ngumu, kesho inaweza kua ngumu Zaidi lakini siku baada ya kesho (keshokutwa) itaanza kua na mafanikio. Hivyo magumu unayoyapitia sasa yanaonyesha kua kule unapoelekea ni kwema. Watu wengi hua wanakata tamaa kesho, wanasahau kua keshokutwa mambo yanakwenda kua mazuri.  Wanasahau kwamba kile walichokua wanakitafuta ndio wamekikaribia.
 Nina neno moja tu la kukwambia usiyaangalie matatizo yako yaangalie maono yako yatazame yale mazuri. Usikubali wakati kama huu uwe karibu na watu ambao wanakurudisha nyuma hata kama ni watu wako wa karibu sana kipindi cha magumu kaa na watu wanaokutia moyo Zaidi maana hutakata tamaa.
Inakwenda kutokea! Ile ndoto uliyoiota kwa muda mrefu sasa inakwenda kutokea ila kama tu hutakata tamaa.
Karibu sana.
Jacob Mushi
0654726668

jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading