Hata ukisoma vitabu 100 vya kuogelea huwezi kujua kuogelea bila ya kuingia kwenye maji. Ili ujue na ufahamu vizuri changamoto zilizopo kwenye maji unatakiwa uingie kuogelea sio kwa kuambiwa na wengine, sio kwa kuuliza. Na hili sio kuogelea peke yake ukitaka kufahamu kitu chochote lazima uingie ndani ufanye katika kufanya utapata uzoefu, ujuzi, na ufahamu zaidi.
Ile biashara uliisikia lakini hadi leo hujaanza hutakaa uijue vizuri kama hutaifanya nenda kawaulize watu 200 waliofanya au walioisikia watakuambia wanayoyajua wao ila ukweli halisi utaujua wewe utakapoanza kufanya na kadiri unavyozidi kuchelewa kuchukua hatua unapoteza muda mwingi na nafasi kubwa ya kujifunza.
Umekutana na fursa nzuri lakini unapata wasiwasi sio vibaya kuuliza kaulize sana ila ukitaka kufahamu vya kutosha ingia ndani ufanye mwenyewe wewe ndie utapata majibu ya uhakika.
Mwanafunzi aliyemaliza chuo na hajawahi kwenda hata field hata kama alipata A masomo yote akienda kutafuta kazi, watamuuliza alishafanya wapi, ana uzoefu gani, uzoefu hauji kwa kusoma vitabu peke yake uzoefu unakuja kwa kufanya, ujuzi unakuja kwa kufanya, acha kusita sita unajipotezea nafasi kubwa ya kujifunza zaidi juu ya fursa uliyokutana nayo. Anza leo hakuna wakati mwingine bora.
Ukisoma vitabu vizuri vilivyoandikwa na watu wenye maarifa makubwa juu ya mahusiano haimaanishi kwamba ndoa/mahusiano yako yatakua bora lazima uingie kwenye mahusiano uanze kufanya kwa vitendo vile ulivyojifunza. Haiwezekani ukaanza leo na ukawa bora leo ni kujifunza kila siku.
Unaanza lini? Anza leo. Unaanzaje na huna mtaji? Mtaji sio pesa tu hata wateja wako wanaweza kua mtaji. Sijaelewa vizuri itakuaje? Utaelewa vizuri zaidi ukiwa kwenye vitendo sio kwa kuambiwa kwa maneno. Sina wa kuniongoza si nitashindwa? Anza utampata anaefanya vizuri hicho unachokifanya na atakusaidia na kukuongoza vyema.
Ni kitu gani ambacho umetamani kukifanya na hadi leo hujakifanya? Unafikiri ni kwanini?
Unaweza kututumia maoni yako kwa kupitia email hapo chini au no ya simu
Asante sana na Karibu kwenye Group letu la Whatsapp kujifunza zaidi
©Jacob Mushi 2016
Niandikie +255654726668 Whatsapp, E-mail jacob@jacobmushi.com
Kujua ni Kufanya.