Watu wengi tumekuwa tu nataka  vitu ambavyo tutafanya tupate matokeo bora peke yake tu.  Kama ni biashara mtu atataka biashara isiyo na hasara yaani yeye tokea ana ianza hadi mwisho asipate hasara yeyote apate mafanikio peke yake.   Ukweli ni kwamba hakuna na kama ipo basi haina thamani kubwa.  Unatakiwa uelewe kwamba kupata faida na hasara ni sehemu katika biashara na hasara mara nyingi huletwa na wewe au nje ya wewe zichukulie hasara kama changamoto ujifunze ili uweze kufanya vizuri zaidi bila kufanya makosa sasa hivi ukiwa unaanza ujue kwamba biashara yako ikikua ukaja kufanya makosa inawezekana ikawa ndio anguko lako na ukapotea kabisa.

Makosa unayoyapitia sasa hivi ndio yatakufanya uwe mtu imara zaidi huko mbeleni. Embu jiulize kama hujawahi kupitia changamoto yeyote ile maishani mwako  unawaeleza nini watu juu ya biashara yako au mafanikio yako?  Ukweli hautagusa wengi hata mimi hutanigusa sitakuamini sana.

Changamoto zinajenga msingi mizuri ya mafanikio yetu changamoto ndii zinatufanya tuweze kusimama imara huko mbeleni. Changamoto ndio inaleta thamani ya kile kitu ulichonacho.  Hujawahi kusikia mtu anasema “angalia usije ukaniharibia hicho kitu nimekipata kwa shida sana”  Chochote kilichopatikana kirahisi hupotea kirahisi vile vile.

Usiogope hasara, usiogope kukosea,  zaidi jifunze kwenye vile unavyopitia utakua mtu mkuu sana.

Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading