Mojawapo ya vitu ambavyo huwarudisha nyuma na kuwafanya wakate tamaa haraka ni kukosa ndoto au kukata tamaa kwenye ndoto zao. Ndoto ni nini? Ndoto ninayoizungumzia sio ile unaota ukiwa umelala bali ni ile ambayo inakufanya usilale.
Kila mtu ana ndoto ya aina yake na za aina mbalimbali mfano unaweza kua na ndoto ya kuishi kwenye nyumba ya aina fulani au unaweza kua na ndoto ya kuendesha gari aina fulani kwa kifupi tunaweza kusema ni vile vitu ambavyo vipo duniani na wewe huna ila unatamani siku moja uje kua navyo.
Vitu hivi ambavyo wewe huna labda ni gari nzuri sana au nyumba nzuri sana au ni maisha ya aina fulani hivi unayataka uyaishi vyoote hivyo vinakuaga ndani ya mtu na mara nyingi ukikaana mtu mkawa na mahusiano mazuri anaweza kukuelezea vile vitu vinavyomfanya afanye kazi kwa bidii.
Ukweli ni kwamba kama wewe unafanya kazi kwa namna yeyote ile ili uweze kutimiza ndoto zako inawezekana endapo hutakata tamaa na kurudi nyuma. Watu wengi wamekua wanakatishwa tamaa na watu ambao wamekua wa karibu zaidi kwako kwa kuwaambia hawawezi na hizo ni ndoto za mchana. Wengine watakwambia ni wewe ukoo wenu wote ni maskini hauna hata wa kukusaidia. Watu wa aina hiyo ni wa kukaa nao mbali kabisa kwa sababu wataua ile ndoto iliyopo ndani yako. Watu wa aina hiyo ni wa kuondoa katika list ya watu unaoshirikiana nao maana wanataka wewe uendelee kubakia kama wao.
Unaweza kulinda ndoto yako kwa kuhakikisha haipiti siku hujafanya chochote ambacho kitakufanya uikaribia ile ndoto yako kama ni kazi au umeajiajiri hakikisha kila siku unafanya jambo la pekee kufikia ndoto zako kwa maana haitatokea tu ghafla umeanza kuendesha lile gari zuri wala kuishi kwenye ile nyumba yako nzuri. Ni kidogo kidogo mpaka unafikia kwenye yale unayotamani yatokee kwenye maisha yako.
Hakuna kisichowezekana kwenye ulimwengu wa sasa endelea kua na ndoto kubwa tafuta watu ambao watakuwezesha wewe ufike kule unapopataka wakuwezesha kwa kukushauri na kukutia moyo kwa namna mbalimbali.
Maisha yako ni vile unavyofikiri. Hakikisha fikra zako zinawaza juu ya maisha unyoyataka. Hujazaliwa hapa duniani ili uje uteseke hadi unakufa nina Imani kwa kuweza kusoma hapa tupo kwenye safari moja ya kufikia mambo makubwa katika maisha yetu.
Linda ndoto yako ione ya thamani na ifanyie kazi kila siku.
Asante sana na Karibu.
Jacob Mushi.