Kila kitu kina kinyume chake hapa duniani, kila kitu kina pande mbili wewe umechagua upande upi? Umechagua kua wapi? Kuna Umaskini na Utajiri, kuna furaha na huzuni, wingi na uchache, kukosa na kupata, Kila unachokipitia sasa hivi kina pande mbili na upande uliopo umechagua mwenyewe inawezekana kwa kujua au bila kujua.

Kwanini uchague upande mbaya au upande ambao kila mtu anauchagua kwanini uishi maisha yasiyofaa wakati kuna upande mwingine wa kuishi maisha unayoyataka? Ni wakati wako kufanya maamuzi na uchaguzi sahihi ni upande upi unataka kuwepo haijalishi upo kwenye hali gani sasa bado unayo nafasi ya kufanya uchaguzi mwingine tena leo, bado unayo nafasi ya kufanya maamuzi mengine tena leo.

Hujazaliwa uwe wa kawaida una nafasi ya kubadilisha hali uliyo nayo maana kila kitu kipo ndani yako, usiangalie hali uliyonayo sasa bali angalia kinyume chake kama huna pesa sasa angalia upande wa pesa jaribu kujenga picha ukiwa na pesa utakua na maisha ya aina gani tofauti na uliyonayo sasa. Kama umefeli shule usiangalie kwamba utaenda wapi angalia uwezo Zaidi ulio nao na unawezaje kuutumia kufanikiwa Zaidi.

Tatizo lolote  unalopitia maishani mwako unaweza kulibadili liwe sababu ya wewe kufanikiwa sana hali uliyo nayo sasa unaweza kuibadili na ukawa katika hali nzuri Zaidi. Kama biashara uliyopo wanafanikiwa wachache kwanini na wewe usiwe katika hao wachache wanaofanikiwa? Amua leo kuchukua hatua na upate kile unachokitaka kwenye maisha yako.

Usichague kukaa upande wa wengi, kitu chochote ambacho ni kirahisi kufanyika hua kinafanywa na watu wengi na mara zote hakina matokeo makubwa. Kama wewe umechagua upande wa watu wengi miasha yako yatakua kwenye hali ngumu.  Kama umechagua kufanya vitu virahisi maisha yako yatakua magumu siku zote.

Nilikua namshirikisha mtu wazo la biashara  nikamaliza akaondoka kwenda nyumbani baadae akanipigia na kuniambia “ Jacob Unaweza kunihakikishia hiyo biashara nikiifanya kwa siku naweza kupata shilimgi mgapi?”  Matokeo ya chochote unachokitaka kwenye hii dunia yanaanza na wewe mwenyewe lazima uamue kukabiliana na changamoto za aina zote utakakutana nazo na wakati mwingine unaweza usipate matokeo unayoyataka kitu kikubwa na cha muhimu ni wewe umechagua nini?

Mtoto anapozaliwa na anapoanza kukaa hadi kutembea na kuongea sio kitu kirahisi tena ukitambua kwamba hajui chochote wala hajawahi kuambiwa unatakiwa utembee au unatakiwa uongee. Kinachomfanya aweze kufanya vyote ni ile hali ya kutamani kutembea na kuweza kuongea. Endapo mtoto anngesema kutembea ni ngumu sana mimi naona sitaweza kutembea hakika angebakia amekaa maisha yake yote. Na wewe ndivyo ulivyoamua kubakia  kwenye hali uliyo nayo sasa.
Unaweza kufanya mabadiliko amua leo.

Asante sana.
Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading