Habari Rafiki, ninayofuraha kukujulisha kwamba Leo ni siku nyingine tena ambayo tumepewa kama zawadi kwa ajili ya kwenda kuyafanya Maisha yetu yawe bora Zaidi. Watakaofanya mambo makubwa leo hawana siku ya tofauti sana na wewe bali watafanya vitu vya tofauti kwenye siku hii.

Jisemeshe Maneno Haya Kabla Hujatoka Kwenda kufanya Chochote.

“MIMI NI MSHINDI SIKU YA LEO, MALENGO YANGU YANAKWENDA KUTIMIA,
KILA NINACHOKIFANYA NINAFANYA KWA UBORA TOFAUTI NA JANA, SITAISHIA NJIANI HADI NDOTO YANGU ITIMIE, EEH MUNGU NIWEZESHE.”

Mojawapo ya vitu vya muhimu sana kwenye maisha yako ni moyo wako.
Moyo wa mtu unapoharibika ndio tunaanza kuona matendo maovu kutoka kwa mtu.

Moyo ubaribikapo mtu hawezi kufurahia chochote alichonacho, iwe ni Mwenza wake, watoto, mali na hata uhai alionao.

Moyo ukiwa Salama ndio utaweza kuitumia vizuri akili yako. Moyo ukiharibika utaitumia akili yako kuleta uharibifu.

Hakikisha siku zote moyo wako haujazwi na chuki, Visasi, Vinyongo, tamaa mbaya, na mengine yote yanayoweza kuleta uharibifu.
Hakikisha una upendo, amani, utu wema, Uvumilivu, kusamehe.

Linda sana moyo wako kuliko vyote uvilindavyo. Moyo wako ndio chemchem inayotoa maji kwenye dunia hii. Ikiingia uchafu wowote watu wataumizwa na maji ya chemchem yako.

NAKUTAKIA KILA LA KHERI
Ubarikiwe sana,
Rafiki Yako, Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading