Kumchukia muovu hakusababishi aache uovu wake bali kuchukia vitendo viovu na kuvikemea. Sisi wanadamu tumekuwa wepesi sana kuwahukumu wenzetu na kuonesha waziwazi kwamba wanastahili kupewa adhabu Fulani kutokana na makosa yao na hata kutaka wauwawe. Ni kweli kuna vitendo havivumiliki kabisa kama mauaji, ubakaji, na mengine mengi.

Hatuwezi kuundoa uovu duniani kwa kuwaua watu wote waovu bali tunaweza kuuondoa kwa kuchagua kutokuwa kama wao. Ukimuua muuaji moja kwa moja na wewe unageuka kuwa muuaji kwasababu hakuna ruhusa ya kuuondoa uhai wa mwanadamu mwenzako tofauti na sheria za nchi.

Njia pekee ambayo unaweza kuitumia kuubadilisha moyo wa mtu muovu ni kuonesha kumjali na kumpenda. Ndio unaweza usinielewe lakini ngoja tuweke katika njia rahisi, mpaka mtu anafikia hatua ya kuchukua silaha na kumuu mwenzake hawezi kuwa mtu mwenye akili timamu, kwasababu akili iliyo timamu haiwezi kukuruhus ufanye hivyo.

Kama ni hivyo basi tunapaswa kuwaona watu hawa kama watu wenye matatizo na wanaohitaji msaada wetu sisi ambao tumeweza kuona wanafanya vitendo visivyofaa. Njia rahisi ni kuwahurumia kuwavuta karibu yetu na kuwapa dawa ya upendo.

Kama ulimpenda mtu sana halafu akakusaliti usimchukie mhurumie muone kama mtu asiekuwa na akili anaehitaji msaada kwasababu angekuwa na akili angegundua na kujali ule upendo uliomuonesha.

Kama mtu amekufanyia ubaya wa aina yeyote hakuna haja ya kujenga chuki na yeye msamehe halafu muonee huruma kwasababu kama akiendelea na hayo atakumbwa na mabaya Zaidi.

Naomba pia utambue kumpenda mtu haina maana ya kwamba uendelee kuwa nae, unaweza kuachana na mtu na bado ukawa unaendelea kumpenda upendo wa agape. Unamuwazia mema katika Maisha yake.

Kumchukia mtu sio tu kumfanyia chochote kibaya unaweza kumchukia mtu kwa kumuwazia mabaya tu. Ukianza kuona unatamani apate matatizo ujue tayari wewe sio mtu mzuri. Na wewe unahitaji dawa.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading