Usijidanganye Ukweli ni Huu.

jacobmushi
1 Min Read
Kama Mwaka 2017  hutakubali kubadilika huwezi kuona mabadiliko chanya zaidi utaona mabadiliko hasi yaani maisha yataendelea kuwa mabovu zaidi.

Kama Mwaka 2017 hutaamua kuanza kujisomea vitabu akili yako haiwezi kukuletea matokeo bora. Lazima ukubali Kuwekeza kwenye akili yako jaza ufahamu ambao utakupa mwanga kule uendako.

Kama wewe upo hapa duniani unawaza kujenga nyumba na kununua gari pekee huo ni uchoyo. Kuna watu wanahitaji kile Mungu alichoweka ndani yako. Gari na nyumba ni vya kwako na wanao. Amua leo uwe na Maono yanayogusa maisha ya wengi.

Kama wewe bado unaona Kujiunga na Semina ni kuwafaidisha watu kamwe huwezi kuendelea kwani hata nguo uliyovaa ulilipia Gharama ndio maana unaitunza. Kitu cha bure mara nyingi wengi hawafanyii kazi. Nina ushahidi watu wengi unaowashauri bure bila gharama huwa hawaendi kufanya chochote.

Kama wewe hadi leo hujatambua Kwanini upo duniani Semina ya Mtandao inayoanza mwanzoni mwa Mwaka 2017 inakuhusu sana ili uweze kuishi maisha yenye maana hapa duniani.

Usikubali kubaki nyuma Jiunge na wenzako tukafanye mabadiliko Mwaka 2017.
Kwa kawaida ada ni ndogo sana tena wakati tunapanga nilitaka kusema watu hawataona kama ina thamani. Lakini wenzangu wakasema tupo kuwasaidia watu tuweke Gharama ambayo kila mmoja anaweza kulipia.

Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone : +255654726668
Blogs: www.jacobmushi.com,  www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading