Kutengeneza Pesa na Kutafuta Pesa. Mojawapo ya njia ya kujitengenezea umaskini siki zote za maisha yako ni kubakia unatafuta pesa maisha yako. Kama unataka ufikie uhuru wa kifedha lazima ujue kuzitengeneza fedha. Tunaposema kutengeneza fedha sio kuwa na mashine inayochapa pesa bali ni kuwa na njia zinazoweza kutengeneza pesa hata kama wewe hutaweka nguvu yako yeyote.

Ukweli ni kwamba kuna nyakati kama unaanza utakuwa kama unatafuta pesa hivi, utatakiwa uweke nguvu nyingi sana. Utatakiwa uweke muda wako mwingi Zaidi. Kuna nyakati itakubidi usahau kulala yaani upate muda mchache sana wa kulala. Kuna nyakati watu watasema uko bize sana umewasahau. Lakini yote haya ni ili uweze kutengeneza mfumo ambao miaka kadhaa ijayo utakuwa unakutengenezea pesa hata kama wewe haupo.

Ni watu wachache sana wenye uelewe huu wa kutafuta pesa na kutengeneza pesa. Kama wewe unapokea kiwango Fulani cha pesa ambacho huna uwezo wa kukizidisha Zaidi ya hapo basi wewe pia unatafuta pesa haijalishi ni kiwango kikubwa kiasi gani. Kama huwezi kusema leo nataka kuongeza hiki ninachopata na kwa juhudi zako ukaweza kukiongeza basi wewe bado upo kwenye kundi la wanaotafuta sio wanaotengeneza.

Ili uweze kuufikia utajiri lazima uingie kwenye kundi la watu wanaotengeneza pesa. Ni safari ndefu kidogo sio siku moja lakini utafika kule unakotaka kufika.

Inawezekana wewe una kipaji chako kizuri sana usiishie kukitumia kipaji pekee jua kuna nyakati zinakuja hutaweza kutumia kipaji chako. Mfano unaweza kuwa mgonjwa, inawezekana ukazeeka na mengine mengi. Lazima ujue ni namna gani unatengeneza mifumo kwa sasa ambayo itakuwa ni mifereji ya pesa huko baadae hata kama wewe hufanyi chochote. Mifumo ii inaweza kuwa ni mojawapo ya kazi zako za kipaji na vitu vingine.

Usikubali kuwa mtu anaetafuta maisha yako yote hapa duniani. Ingia kwenye kundi la wanaotengeneza. Huku ndipo wapo watu wanaofurahia kuwepo hapa duniani.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading