HATUA YA 306: Vinavyotokea Vyenyewe.

Vitu vinavyotokea Vyenyewe Kwenye Maisha yako mara nyingi ni vitu ambavyo Huvihitaji, na wala havina mchango chanya kwako, ni kama magugu ndani ya shamba. Kutarajia vitu vitokee kwenye Maisha yako na hujaweka juhudi zozote basi ujue kitakachotokea hakina tofauti na magugu.

Usipojitoa kupata kile ambacho unakitaka utajikuta siku zote matokeo unayopata sio yale ambayo unatamani yatokee kwenye Maisha yako. Lazima ukubali kuweka juhudi Zaidi ya pale ambapo umezoea kufika.

Ili uweze kukua Zaidi yah apo ulipo sasa hivi unapaswa kufanya Zaidi ya unavyofanya siku zote. Unapaswa kujaribu vitu ambavyo hujawahi kabisa kufanya.

Ukuaji hautokei wenyewe lazima kuna mahali uhusike katika kuweka juhudi.

Vitu vile ambavyo tumezoea kuviona vinatokea vyenyewe bila ya juhudi kubwa kuwekwa havina manufaa makubwa katika ukuaji wako.

Mara zote utaishia kuwa mtu wa kawaida kama watu wengine. Kama wewe umeamua kukaa na kumsubiria mteja atokee na hakuna juhudi nyingine ya ziada unayoweka utaendelea kupata matokeo yale yale ya siku zote.

Chagua kwenda Hatua nyingine Zaidi fikiri tofauti na wengine wanavyofikiri ndipo utaweza kusonga mbele Zaidi ya wengine.

 

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

 

This entry was posted in HATUA ZA MAFANIKIO and tagged on by .

About jacobmushi

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *