Huwezi kuondoa chuki kwa kuchukia, kama mtu akikutendea ubaya wewe ukimtendea ubaya unakuwa huna tofauti na yeye. Huwezi kuzima moto kwa kuuongezea vichocheo vinavyoufanya uendelee kuwaka.
“The best revenge is not to be like your enemy.”
― Marcus Aurelius, Meditations
Mwanafalsafa huyu Marcus aliwahi kusema “Kisasi cha kweli ni kutokuwa kama adui Yako” Yaani watu wanaopambana kukuangusha usiwalipilize kwa kuwaangusha fanya jambo ambalo litakuweka tofauti na wao.
Yale mabaya watu waliokufanyia hayapaswi kukubadilisha wewe kuwa mtu mbaya Zaidi. Mabaya yanapaswa yakutengeneze uwe mtu ambaye ni tofauti na wabaya wako.
Usipoteze muda wako kufikiri juu ya kuwaaibisha watu ambao wanakuchukia endelea kuwa mwema na kuwapenda.
Kama ulikuwa kwenye mahusiano ukasalitiwa, ukibadilika ukawa msaliti Zaidi unakuwa hujafanya jambo lolote la tofauti. Wewe pia unakua ni msaliti.
Usifanye makossa kwasababu kuna wengine wanafanya makossa Zaidi.
Hakuna sehemu yoyote duniani waliwahi kupongezwa watu ambao wameweza kulipa kisasi na kuwapoteza kabisa maadui zao.
Ukweli ni kwamba wanaolipa kisasi kibaya wanakuwa wameshindwa kudhibiti hisia ambazo zilizoko ndani yao.
Kingine ambacho hupaswi kukisahau kama utatenda ubaya kwa aliekutendea ubaya wewe unaonekana ni dhaifu kuliko hata yeye aliekutendea ubaya. Ukiweza kusamehe unakuwa na uimara Zaidi yake.
Tenda wema kila wakati bila kujalisha ni nani unamtendea wema.
Ni mimi Rafiki Yako,
Jacob Mushi
USIISHIE NJIANI
Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/