Kuna mambo ambayo tunafanya sasa wakai mwingine tunaweza kuwa tunabishana sana juu ya nani yupo sahihi na nani amekosea. Ukweli unaweza usielewe kwa haraka kwasababu wengi wanaweza kutumia mapenzi binafsi na kuangalia kile wanachokipata kwa wakati huo.

Mambo mengine yakiwa magumu katika kuujua ukweli tunaachia muda kadiri muda unavyokwenda ndio tutajua nani alikuwa mkweli na nani alikuwa anaudanganya. Wako watu wanaweza kutete jambo Fulani ni sahihi na wakatoa na uthibitisho wa usahihi wake ila tukiachia muda utupe majibu ndio tunaweza kuwa na uhakika.

Kila jambo lina matunda yake, tukiona matunda ndio tutajua huu ni mlimao au ni mchungwa, hatuna haja ya kubishana kwasababu tumeona miiba kwenye mche ukiwa mdogo. Wewe uliekuwa unatetea kwa nguvu kwamba huu ni mchungwa tutajua ukweli tutakapoona matunda ya ule mti. Ulietuambia kwamba huu ni mlimao tutajua ukweli matunda yakitoka.

Itakuwa ni aibu sana kwa wale waliokuwa wanatumia nguvu kubwa sana kuutetea uovu ambao ulikuwa wazi kabisa. Itakuwa ni aibu sana kwa wale waliotumia uwezo wao wa akili mpaka mwisho kuwalazimisha watu waamini juu ya jambo ambalo lililokuwa linaonekana wazi kwamba ni ovu.

Ni vizuri tukajua kwamba baada ya Maisha yetu hapa duniani kuna kizazi kingine kitakuwepo, bahati mbaya sana tunayofanya sasa hivi yanatunzwa kwenye kumbukumbu. Wajukuu zetu watakuja kusema babu zetu walikuwa na akili lakini walifanya mambo yakipumbavu sana. Babu zetu walipewa madaraka makubwa na uongozi mkubwa lakini walifanya mambo yakitoto kabisa.

Ni vyema sana tutazama mbele yaani kwa maana ya dunia inayokuja itakuta tumetengeneza aina gani ya Maisha kwa ajili yao. Tunapofanya mambo kwa ajili yetu sasa hivi ni vyema tulkafikiri pia ni kwa namna gani yanaathiri kizazi kijacho na sio kuangalia zile faida zetu tunazopata kwa wakati tukiwa hapa duniani tu.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading