Bila picha hakuna mwelekeo.
Bila Picha hakuna maisha.
Bila picha utachukuliwa na kila kinachokuja.
Bila Picha hakuna maisha.
Bila picha utachukuliwa na kila kinachokuja.
Picha inakupa mwongozo,
Picha inakupa vipaumbele.
Picha inakupa uwezo wa kuchagua marafiki.
Picha inakupa hamasa.
Picha inakupa ujasiri.
Picha inakupa uwezo wa kujieleza.
Picha inakupa vipaumbele.
Picha inakupa uwezo wa kuchagua marafiki.
Picha inakupa hamasa.
Picha inakupa ujasiri.
Picha inakupa uwezo wa kujieleza.
Kama huna picha ya maisha yako ya baadae utayumbishwa sana na mambo yanayoendelea duniani.
Kwenye Dunia hii kila mtu anatamani uwe naye hivyo kama wewe huna picha maisha yako yataingiliwa na kila mtu.
Kama huna picha vipaumbele vya watu wengine vitakuchukua, watu watakupa majukumu yao uyafanye. Hujawahi kusikia mtu anakuletea biashara fulani Nzuri inalipa sana itatuwezesha ujipatie pesa na mali za haraka, ukishajiunga unakutana na picha ya tofauti. Unakuta kumbe ni lazima uweke bidii sana ili upate yoote yale uliyoonyeshwa.
Kama una picha ya maisha yako ya baadae Utaweza kujua marafiki ulionao ni wapi wa kuondoa, na ni wapi wa kubaki nao.
Utaweza pia kujua ni maisha ya namna gani uishi sasa hivi ili uweze kutengeneza baadae yako nzuri. Kila unachokifanya sasa hivi kina mchango fulani kwenye kesho yako.
Kama una hali mbaya sasa hivi kuna mahali hukufanya Vizuri siku zilizopita. Ili uwe na baadae Nzuri fanya mambo yanayotakiwa ili ujitengenezee matokeo bora ya baadae.
Picha ni maono. Mtu ambae hana maono biblia inasema huacha kujizuia. Yaani maana hawezi kujua ni kipi kinafaa kufanya na kipi hakifai kufanya. Kama huna maono Huwezi kujua ni kipi cha kuanza sasa hivi na kipi cha kufanya baadae.
Unajenga nyumba ukianza kununua vyombo vya ndani kama masofa, friji n.k, halafu ukavileta kwenye kiwanja tutakuona kichaa. Hivyo kuna watu maisha yao yako hivyo. Wanaanza kuigiza maisha ya baadae sasa hivi.
Kama huna picha ya maisha yako, Huna mwelekeo wa maisha yako.
Jacob Mushi