Usiwaweke wengine juu kwa yale mazuri waliyonayo na wewe ukajiweka chini. Hata wewe una vitu vizuri pia ndani yako. Usijisikie vibaya kwa kuona zile zawadi zilizoko kwa wengine ukasahau kwamba na wewe pia una zawadi nyingi ndani yako.

Una vipaji ndani yako, Mungu amekuumba uweze kutumia vitu hivyo hapa duniani. Usijiweke chini kwasababu unawaona wengine wanafanya vizuri kuliko wewe.

Kila mmoja ana sehemu yake ambayo ni bora. Kila mmoja ana jambo ambalo analiweza vizuri kuliko mtu mwingine yeyote hapa duniani. Hivyo basi ukiona mtu anafanya vizuri kwenye sehemu yake usijisikie vibaya na kujiona chini.

Usijisikie vibaya pia pale unapoona hakuna mtu anajali kile unachokifnaya wewe endele kufanya vitu sahihi. Usiwalazimishe watu wakupende wewe endelea kufanya vitu sahihi utawavuta watu sahihi kwenye Maisha yako.

Maisha yako yamebebwa na vile vitu ambavyo Mungu ameweka ndani yako. Sababu ya wewe kuendelea kuwa hai mpaka sasa ni kwasababu kuna vitu hujavitumia bado ndani yako. Jiamini na chukua Hatua.

Wewe ni mtoto wa Mungu hivyo jiamini kama alivyo baba yako aliekuumba.

Nena mazuri juu yako kila wakati na popote pale ambapo unakuwa. Usikubali kusema siwezi hili na hili sema vile unavyoviweza.

 

Nakutakia Jioni Njema,

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading