Njia pekee ya kupata juice ya nanasi ni kulisaga na kulikamua nanasi. Kwa kawaida inaonekana kama ni kuharibu lakini ndio njia ya kupata juice.

Kuna mambo yanatokea kwenye maisha kwa nje yanaonekana ni mabaya sana. Kwa nje inaonekana kama umepigwa na Mungu.

Nataka nikwambie kuna kitu kipya kinakuja baada ya hayo unayopitia. Kuna bidhaa mpya ambayo watu wataifurahia baada ya yale unayopitia.

Kuna mtu mpya anatengenezwa kwa kupitia changamoto ulizonazo. Huwezi kuiona juice ya nanasi bila kuliharibu nanasi. Kama utaendelea kulihurumia nanasi litaoza

Sio rahisi unielewe lakini ipo siku utakuja kunielewe Ukishapita hapo unapopita sasa.

Baada ya hayo unayopitia hutakuwa wewe tena, utakuwa kama bidhaa mpya yenye thamani Zaidi, kutoka nanasi lililokuwa limetupwa chini hadi kuwa juisi ambayo inawekwa kwenye glasi yenye thamani kubwa.

Biashara yako itakwenda kukua Zaidi, thamani yako kazini itakwenda kuongezeka, unakwenda kulipwa Zaidi, unakwenda kuwa wa maana Zaidi.

Usikate tamaa, endelea kuvumilia kwani bado kidogo furaha yako inakuja tena, bado kidogo unakwenda kutabasamu tena.

Lipo Tumaini Tena, Usiishie Njiani.

​www.jacobmushi.com/coach

7 Responses

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading