HATUA YA 349: Umeshawahi Kukutana na Mtu wa Aina Hii?

Soma Vitabu Hivi; MAFANIKIO KWENYE BIASHARA SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO USIISHIE NJIANI TIMIZA NDOTO YAKO. MBINU 101 ZA MAFANIKIO UMUHIMU WA MAONO. Kuna aina mbalimbali za watu hapa duniani wenye kila aina ya tabia. Kuna aina ya watu ambao ukikutana nao ukakaa nao dakika chache unapoteza mwelekeo kabisa wa Maisha yako. Watu hawa […]

HATUA YA 348: Hii Ndio Njia Bora Kupima Mafanikio Yako.

Mara nyingi tumekuwa tunafanya mambo kwasababu ya mifumo tuliyoikuta na kuambiwa ni sahihi lakini si kweli. Ukiwa shuleni mnapewa mtihani mmoja wanafunzi 100 na mnapimwa viwango vyenu vya mafanikio kwa mtihani mmoja. Lakini ukweli ni kwamba unaweza kupata sifuri kwenye mtihani lakini bado kuna jambo jingine unaweza kulifanya vizuri kuliko wale wenzako 99. Inawezekana wewe […]

HATUA YA 347: Vita Inapokuwa Ngumu..

Ukiona ugumu unazidi tambua ya kwamba ndio mwisho wa pambana unakaribia. Ukiona changamoto zinazidi kuwa nyingi basi ujue kuna sehemu unakaribia kuvuka. Mbegu ikifukiwa chini baada ya muda huanza kuota wakati wa kuota sio wa mchezo. Ni mapambano kati ya mbegu inayojitoa kutoka kwenye maganda yake na kukutana na ardhi kwa juu. Lazima ikubali kusukuma […]

HATUA YA 346: Unaweka Mchanganyiko Sahihi?

#Maji ni kimiminika ambacho kinatumika katika vitu vingi sana kwenye Maisha yetu. Ili uweze kuyatumia maji lazima uwe na lengo la kuyatumia la sivyo unaweza kuwa na maji na yasiwe na kazi. #Maji ukichanganya na sabuni unapata povu la kufulia nguo. Maji hay ohayo ukiyachanganya na sukari na majani ya chai kisha ukayachemsha unapata chai. […]

HATUA YA 345: Mambo Ambao Wengi Wanakwepa Kufanya.

Kwenye dunia kila mmoja analipwa kwa thamani anayoitoa. Aina ya Maisha unayoishi ni kutokana na thamani unayoipa dunia. Mshahara unaolipwa ni thamani unayoitoa kwa bosi wako. Makossa utakayokuwa unafanya ni kusahau kwamba thamani inaongezwa, na kama inaongezwa basi ujue hiyo uliyonayo kuna kipindi itashuka kama isipoongezwa. Yapo Mambo Ambayo unapaswa Kufanyia kazi Kila Wakati kwenye […]

HATUA YA 344: Kuna Kinachobadilika?

Kama kuogopa kwako hakubadilishi chochote kwenye kile unachokiogopa hakuna maana ya kuogopa. Hakuna haja yeyote ya kuwa na woga ama wasiwasi kwasababu hakubadilishi matokeo yeyote katika yale tunayoyaogopa. Kama umeambiwa mafanikio sio rahisi na ukaingia huku una hofu kubwa na mawazo juu ya ugumu ni sawa na kupoteza nguvu zako bure kwasababu kuogopa huko hakubadilishi […]

HATUA YA 343: Unalofanya leo, matokeo ni kesho..

Dada mmoja alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni kubwa sana sehemu ya mapokezi. Kazi ile ilimpa kiburi sana kwasababu ilikuwa ni kampuni ambayo ina jina kubwa sana. Alikosa adabu kabisa kwa watu ambao hawajui ana alionyesha dharau waziwazi. Kwa unafiki mkubwa alijifanya anawahudumia vizuri sana wale watu wakubwa ambao aliwajua majina na vyeo vyao. Baada ya […]

HATUA YA 342: Unaemngoja Anakungoja Wewe.

Inawezekana kuna mtu unamngoja aje afanye jambo kwenye Maisha yako ili yabadilike. Inawezekana kwenye akili yako unasubiri ipo siku mambo yatakaa sawa na kuwa marahisi Zaidi ya sasa. Inawezekana pia kuna muujiza Fulani unautegemea kwenye akili yako utokee ndio kila kitu kibadilike kwenye Maisha yako. Napenda kukwambia Rafiki huyo unaemngoja afanye yote hayo anakusubiri wewe […]

HATUA YA 341: Kwenda na Wakati.

Kila mmoja anatamani sana kwenda na wakati, hakuna anaetaka kuonekana yeye ni wa zamani. Hii ndio maana unakuta watu wanakimbizana na mitindo mbalimbali mipya ya mavavi. Simu mpya, magari mapya na vitu kadha wa kadha. Tatizo linakuja pale ambapo unajitahidi sana uende na wakati kwa nje lakini unasahau ndani yako. Unaposahau ndani ukabaki unapamba nje […]

HATUA YA 340: Vitu Hivi Viko Sambamba Siku Zote.

Huwezi kusema unataka mwili wenye misuli bila ya mazoezi magumu na mazito. Huwezi kusema unataka mtoto lakini hutaki kubeba majukumu ya kupata mtoto. Maumivu, kukataliwa, kupingwa, kusemwa vibaya, kuonekana umechanganyikiwa ni dalili zinaonyesha kwamba kile unachokifanya kina matokeo makubwa sana na hakijawahi kufanywa na wengine. Dalili ya kwanza ya kujua kule unapoelekea ni kwa namna […]