HATUA YA 339: Ukisubiria Nafasi Itokee, Wenzako Wanatengeneza Nafasi.

Kwenye Maisha unapaswa uweze kutofautisha kati ya vitu ambavyo unatakiwa uvifanye vitokee na ambavyo unatakiwa usubiri vitokee kwa uweza utokao juu. Ukishindwa kuvitofautisha hivi unaweza kukuta unateseka sana kwenye mambo ambayo ulipaswa kufanya mwenyewe. Unapoteza muda kwenye vitu ambavyo havipo kwenye uwezo wako wa kuvifanya vitokee. Ukiwa na vipaji vizuri vya uchoraji ukachora picha ukaziweka […]

HATUA YA 338: Jua Kusudi Lako, Ili Usiteseke na Majira ya Wengine.

Kama tunasema kila binadamu ana upekee wake basi ni kama zilivyo mbegu za mimea mbalimbali. Kila mbegu ina muda wake wa tofauti katika kuonekana imeanza kuchipuka kutoka ardhini. Ukipanda mahindi au maharage unaweza kutegemea kuuona mmea umeanza kuchipuka siku ya tatu hadi saba. Lakini tukija kwenye mimea mingine kuna ambayo hupita muda mrefu sana hadi […]

HATUA YA 337: Hakuna Kinachotokea Bila Ya Sababu Hata Kama ni Kibaya.

Unapoona mabaya yamekuja kwako usiwe mwepesi wa kulalamika bali penda kujiuliza maswali. Penda kudadisi ni wapi umekosea au ni kitu gani unapaswa kujifunza. Umeingia kwenye mahusiano na mtu na mkajikuta mnashirikiana kwenye mambo mengi kwa pamoja. Maono yenu mkaweka pamoja, na baadhi ya mambo mkaanza kufanya pamoja. Mnakuza vitu pamoja hadi mnafikia Hatua ya kubwa […]

HATUA YA 336:  Kwenye Dunia Unayoweza Kuwa Chochote Unachotaka.

Kwenye dunia hii ambayo kila unachotaka kuwa unaweza kuwa ni vyema ukachagua kuwa mwema. Hii ndio njia pekee ya kwanza kuonyesha wewe ni binadamu. Mtu anapofanya jambo baya la kikatili kuna usemi hutumika “amefanya jambo la kinyama sana” yaani maana yake wewe kama binadamu tofauti yako na Wanyama wengine ni ule utu ulioko ndani yako. […]

HATUA YA 335: Hamasa Yako ya Ndani Inaletwa na Nini?

Kila mtu kulingana na kile anachokitaka kuna namna anakuwa na hamasa ndani yake. Swali la kujiuliza ni kitu gani hasa kinakupa hamasa? Kitakachoamua udumu kwenye maamuzi uliyofanya ni kile chanzo cha hamasa yako. Kitakachoamua uweze kushinda changamoto ni kile chanzo cha hamasa yako ya ndani. Kama ndani yako hakuna kitu kinachokusukuma kufanya kama vile vya […]

HATUA YA 334: Ukitaka Kuwa Mkubwa wa Wengine Kubali Hiki..

Kanuni ya kuwa Mkubwa wa wengine siku zote ni kutumika. Hakuna bosi alieweza kuajiri maelfu ya watu kwenye kampuni yake kama hakutoa muda wake akitumika hadi akafikia uwezo wa kuajiri. Hakuna aliefikia mafanikio makubwa na kujulikana na wengi kama hakutoa nguvu zake katika kuonyesha ule uwezo uliokuwa ndani yake. Hata kama una sauti nzuri ya […]

HATUA YA 333: Usipoteze Muda Kwenye Kitu Hiki Kabisa.

Tunayaelewa mambo kulingana na uwezo wetu wa kufikiri na namna mitazamo yetu ilivyo. Kama ni hivyo basi utakuwa ni upotevu wa muda usio na msingi kabisa kama utakaa kwenye kundi la watu ukibishania, mpira, siasa, dini, au kitu kingine chochote. Kila mtu anaweza kutetea kile alichokiamini, sio rahisi ubadilishe Imani ya mtu kwa maneno matupu […]

HATUA YA 332: Unajijengea Ukuta Au Unafungua Njia?

Katika Maisha yetu ya kila siku na vitu tunavyofanya kuna kitu ambacho tunatengeneza. Vile unavyoishi Maisha yako kuna picha watu wanaijenga kuwa wewe ndio hivyo ulivyo. Vile unavyoongea kuna picha watu wanajenga kwenye akili zao kwamba wewe ndio hivyo upo. Kama unaongea maneno ya hovyo picha itakayojengeka ni kwamba wewe ni wa hovyo. Kama utakuwa […]

HATUA YA 331: Ukielewa Hili Huwezi Kuwa na Maumivu Ndani ya Moyo.

“We suffer more often in imagination than in reality” ― Seneca Mara inaweza kuwa jambo dogo sana limetokea mahali lakini kwa kupitia fikra zetu tukajikuta tumekuza lile jambo na kuendelea kupata maumivu makubwa. Mwanafalsafa Seneca anasema tunateseka Zaidi katika vitu tunavyovifikiria kuliko vile vitu halisi. Mfano mdogo ni pale umempigia mtu simu hakupokea au akaikata unaweza […]

HATUA YA 330: Kinachokufanya Uogope Kifo Ni Kipi?

Katika mambo ambayo kila mwanadamu ana uhakika kwamba lazima yatokee kwenye Maisha yake mojawapo ni kifo. Kila mmoja anajua kwamba ipo siku ataondoka duniani, japokuwa hakuna ajuae ataondoka siku gani na kwa njia ipi. Kinachoshangaza sana ni watu ambao wanakuwa na hofu sana wakiwaza juu ya kifo au siku ya kufa kwao. Hii inatokana na […]