Connect with us

HATUA YA 255: Unataka Kwenda Hatua Nyingine?

HATUA ZA MAFANIKIO

HATUA YA 255: Unataka Kwenda Hatua Nyingine?

Unataka Kwenda hatua ya juu Zaidi? Lazima ukubali kupitia mitihani ya kukupima kama unaweza kukaa kwenye hatua inayofuata. Kama hutaki kupita kwenye mitihani huwezi kupanda hatua nyingine. Kama hutaki kupimwa hutaweza kuingia kwenye hatua za juu Zaidi utabaki hapo ulipo kwa muda mrefu Zaidi. Ukiona unabaki sehemu moja muda mrefu kuna uwezekano kuwa unafeli mitihani. […]

Unataka Kwenda hatua ya juu Zaidi? Lazima ukubali kupitia mitihani ya kukupima kama unaweza kukaa kwenye hatua inayofuata.

Kama hutaki kupita kwenye mitihani huwezi kupanda hatua nyingine.

Kama hutaki kupimwa hutaweza kuingia kwenye hatua za juu Zaidi utabaki hapo ulipo kwa muda mrefu Zaidi.

Ukiona unabaki sehemu moja muda mrefu kuna uwezekano kuwa unafeli mitihani. Kama sio kufeli basi kuna mitihani unairuka.

Haiwezekani hata siku moja ukataka kupata mtoto lakini unagoma kubeba ujauzito. Unataka pesa lakini hutaki kufanya kazi ya kukutengenezea kipato hicho.

Unatakiwa ujue kabisa gharama unazotakiwa kulipa kabla hujatamani hatua ambazo wengine wamefikia au ile hatua unayotaka kufika.

Kwa kulipa gharama pekee ndio tunaweza kutoka sehemu tulipo na kwenda sehemu nyingine kubwa Zaidi.

Watu wengi sana wanaishia kusema wanataka vitu Fulani na Fulani lakini wanakwama ile sehemu ya kulipia gharama.

Wengi sana wataweza kuona ndoto kubwa, kuwaza makubwa kusema makubwa lakini ni wachache wako tayari kulipa gharama, kuvumilia, kupokea kila hali ambayo inaweza kutokea njiani.

Chochote unachokitaka lazima ukubali kulipia gharama zake. Ukitaka ukubwa kuna gharama za ukubwa na uwe tayari kubeba changamoto zitakazotokea kwenye ila hatua unayoifuata.

Wengi wanataka kuwa viongozi lakini hawataki kubeba lawama, kukosolewa, kulalamikiwa, au kusemwa na wale wanaowaongoza. Unachotakiwa kila hatua unayotaka kupanda lazima ukubali kuwa mvumilivu.

Kwa kulipa gharama pekee ndio tunaweza kupata kila tunachokitaka. Wako waliokubali kudharaulika kwa muda lakini sasa hivi dharau wanazisimulia kama hadithi tu.

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako”

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in HATUA ZA MAFANIKIO

To Top