Habari rafiki, leo tunakwenda kuona njia za kugusa maisha ya wengine ili tuweze kufikia mafanikio ya kweli.  Kwenye kila kitu ambacho Mungu ameweka ndani yako ni kwa ajili ya wengine. Kama utaweza kukitumia vyema utakuwa umeweza kuyasaidia maisha yako mwenyewe.

Maana ya kugusa maisha ya wengine.

Kugusa Maisha ya wengine ni kile kitendo cha kuongeza thamani kwenye Maisha ya watu. Ni kitendo ya kuyafanya Maisha ya wengine kuwa marahisi au kuwasaidia waweze kufurahia Maisha yao hapa duniani.

Kama kile unachokifanya kinayafanya Maisha ya wengine kuendelea kuwa bora wewe unayagusa Maisha yao.

  1.  Kwa nini ni muhimu kugusa maisha ya wengine.

Ni muhimu sana kugusa maisha ya wengine kwasababu hicho ndio kitu pekee cha kutuwezesha kuacha alama duniani.

Watu wote tunaowakumbuka waligusa maisha yetu kwa upande chanya kupitia yale waliyokuwa wanayafanya.

Maisha yetu yatakuwa na furaha na amani  kama tutayagusa maisha ya wengine.

Hakuna binadamu ambaye ana furaha kwa kuwaumiza wengine  unapogusa wengine  kwa kazi yako au biashara yako moja kwa moja unapata amani.

  1.  Kugusa maisha ya wengine kupitia kazi yako.

Haijalishi unafanya kazi ya aina gani bado una nafasi ya kugusa maisha ya wengine endapo tu kazi yako inaongeza thamani kwenye maisha yao.

Unapoongeza kiwango cha Thamani  inayotoa kazi yako ndipo MAFANIKIO yako huongezeka.

Kama wewe ni mwajiriwa mwajiri wako anakuwa ameguswa na wewe kwasababu ya uwepo wako pale kazini. Kile ulichonacho unapokitoa kwa ajili ya yule aliekuajiri ndipo na wewe unapokea.

Unapata nafasi ya kugusa maisha ya wafanyakazi wenzako kwa kufanya kazi kwa bidii na kuwa mfano wa kuigwa.

  1.  Kugusa maisha ya wengine kupitia biashara yako.

Kwa kupitia biashara yako kuna maisha ya watu wengi sana unayafanya yawe bora.

Inawezekana unazalisha bidhaa zako. Mwenyewe au unanunua bidhaa na kuziuza. Yote kwa pamoja unagusa maisha yao,  labda wengine ni kila siku wanakuja kwenye biashara yako ili kupata kile unachotoa maisha yao ili yaende sawa lazima waje kwenye biashara yako.

Kadiri unavyoongeza idadi ya watu wengi unaowagusa ndio mafanikio yako yanaongezeka. Sehemu ya muhimu unayotakiwa kufanya kwa bidii ni kuwapa kile wanachohitaji kwa moyo wako wote.

Kamwe usije ukajisahau kwamba maisha yako ili yawe bora ni pale utakapofanya maisha ya wengi yawe bora zaidi kwa kupitia biashara yako au bidhaa zako.

  1.  Kugusa maisha ya wengine kupitia kipaji chako.

Labda wewe ni mwimbaji,  muigizaji,  mchekeshaji,  mchezaji na nyingine unazozijua.  Unagusa maisha ya watu wote wale ambao wanapendelea kile unachokifanya.

Kwa kupitia kipaji chako kuna watu wanapata burudani na faraja ndani ya mioyo yao.

Kuna watu wanatumia sehemu ya maisha yao kwa ajili ya kukufuatilia wewe.

Kuna watu hawawezi kuishi maisha yao wakiwa na furaha bila kusikikiliza au kuona unachokifanya.

Ongeza bidii  usiogope utafikia ndoto yako ya kugusa maisha ya wengi zaidi.

  1.  Kugusa maisha ya wengine kupitia huduma unazotoa.

Kwa kupitia huduma yako unayotoa unarahisisha maisha ya wengine. Unatatua matatizo ya wengine.

Kama unatoa huduma ya usafiri unatatua tatizo la umbali au uchovu kwa watu ambao wangetembea na miguu. Kwa kutatua tatizo hili unakuwa umegusa maisha yao.

Wanafurahia maisha kwa kupitia huduma yako.

Sehemu ile uliyopo una watu wengi ambao unawagusa hakikisha unawafahamu vizuri ili uweze kugusa maisha yao vizuri.

  1.   Changamoto unazokutana nazo kwenye kugusa maisha ya wengine na namna ya kuzivuka.

Changamoto unazokutana nazo kwenye kugusa maisha ya wengine.

Kwanza kabisa haupo mwenyewe kwenye chochote unachokifanya hivyo kuna wakati  utapata ushindani na wewe kushindwa kutimiza malengo yako.

Hapa unatakiwa uwe na ubunifu na utofauti na wengine maana hicho ndio kitawafanya watu waje kwako. Zitambue sababu a watu kuja kwako na sio kwa wengine.

Kupata hasara, mfano ni biashara unaanzisha inakufa.

Usikate tamaa kama hicho ndio kinausukuma moyo wako anza upya, jifunze mbinu na njia mbalimbali mpya.

Kukatishwa tamaa, kuna watu wengi watakwambia unapoteza muda, wapo walioshindwa,  kafanye kitu kingine na mengine mengi.

Usikubali kuacha kufanya jambo lile linalotoka moyoni mwako kwasababu kuna watu wa nje wanakwambia huwezi.

Unachotakiwa utambue zaidi ni kwamba yote haya tunatatua matatizo ya wengine. Kwa kutatua matatizo mengi ndio unaweza kutatua matatizo yako.

Tunachotakiwa kufahamu ni kwamba kila analo jukumu la kuhakikisha  kuna watu sehemu mbalimbali ambao maisha yao yanaguswa kwa kupitia kile unachokifanya.

Ikiwa ni bidhaa yako,

Ikiwa ni kipaji chako,

Ikiwa ni huduma unazotoa,

Ongeza wigo zaidi kwasababu muda ni mchache na hakuna nafasi ya kupoteza muda.

Unapoamka asubuhi  jiulize siku yangu ya leo ni watu wangapi wanakwenda kuguswa na hiki ninachokifanya?

Usikubali siku ipite bila kufanya maisha ya mtu mmoja kuwa bora au kuwa na  thamani zaidi.

Usiishie kutumia vya watu pekee kuwepo na kitu chako huku duniani ambacho watu wanafurahia kukitumia.

 

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading