Category Archives: BIASHARA NA UJASIRIAMALI

#KONA YA BIASHARA: Unachoweza Kufanya Ni Kipi?         

Unaweza kuwa na sababu za kila aina zinazoelezea kwanini hadi sasa huna unachokifanya au hujamiliki biashara yako. Swali langu kwako litakuwa ni unachoweza kufanya ni kipi? Tukiacha hizo sababu unazotoa je hakuna hata kitu kimoja kidogo unaweza kufanya? Hakuna kweli? Hakuna unachojua Zaidi ya wengine hapo mtaani kwenu kweli? Hakuna biashara inayoendeshwa hovyo hovyo hapo mtaani uende ukakae nao ufanye vitu vya tofauti hadi wakuambie ujiunge nao kweli? Sasa utakuwa unafanya nini hapa duniani kama hakuna hata kitu kimoja unachoweza kufanya vizuri Zaidi ya wengine wachache waliokuzunguka?

Inawezekana huna hela kabisa hapo ulipo lakini unaweza kuzungumza na watu vizuri ukawashawishi. Hapo mtaani kwenu kuna mama anauza maziwa ya mtindi lakini hajui kuyauza vizuri wala kushawishi watu. Wewe tumia uwezo wako wa kuongea na watu na kuwashawishi uuze maziwa kama kwenye kila lita moja ya maziwa ukiweza kutengeneza sh 300 hadi 500 sio sawa na ambaye hana kazi ya kufanya.

Rafiki yangu mmoja akaniambia yeye alikuwa chuo kikuu na hakubahatika kupata mkopo. Aliishi kwa shida sana hadi siku moja alipopata wazo la biashara. Pale alipokuwa ananunua chakula kila siku kwa tsh 2,000 aliamua kuongea na yule mama muuzaji. Akamwambia nitachukua sahani kumi kila siku jioni lakini utakuwa unaniuzia kwa sh 1500. Yule mama akakubali mwanafunzi yule akawafata marafiki zake aliokuwa anaishi nao akawaambia nitakuwa nawaletea chakula hapa kila siku jioni.

Wenzake wakakubali ikawa kwenye kila sahani kumi anatengeneza tsh 5000. Akaongeza bidii akaweza kuwahudumia wengine hadi sahani 20 kila siku jioni. Aliendelea na biashara ile kwa ule muda wake wa ziada wa jioni kila siku na akapata pesa ya kuendeshea Maisha na mahitaji mbalimbali aliyokuwa nayo.

Kuanza biashara unaweza kuanza kwa namna yeyote ile inategemea tu na mtazamo wako ulivyo. Kile unachokijua ukiweza kukitumia vizuri kitakutoa.

Jifunze kuuza, ukishajua kuuza tafuta bidhaa ambayo utaijua vizuri sana kisha utafute wateja wake. Hakikisha una uhakika wa upatikanaji wa bidhaa unayotaka kuuza. Tafuta wateja kachukue bidhaa peleka kwa wateja wako. Unaweza kutengeneza faida kidogo lakini sio sawa na mtu ambaye hauzi chochote, au anaelalamika hana kazi wala biashara.

Huo unaweza kuwa mwanzo wako mdogo lakini una malengo makubwa ya kuja kumiliki biashara yako mwenyewe. Mawazo ya biashara yapo mengi sana na unaweza kuanza kwa namna ya ajabu sana lakini hakuna watu wanaoweza kuwa na fikra chanya za kugundua hayo.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

KANUNI 10 ZA MAFANIKIO ANAZOPASWA KUZIJUA MJASIRIAMALI.

Habari rafiki, leo kwenye ujasiriamali tunakwenda kujifunza juu ya kanuni 10 ambazo unapaswa kuzijua wewe mjasiriamali. Ni imani yangu kwa kupitia makala hii utatoka na mwangaza kwenye kile unachokifanya. Kila mmoja anamtegemea mwenzake, kwa kupitia unachokifanya kuna watu wamerahisishiwa maisha yao. Wewe pia kuna watu wengi sana wanahusika kukufanya wewe uishi kwa urahisi. Ni muhimu kuwa mwema kwa kila mmoja wetu.

1.Kuwa Mtatua matatizo

Ili uweze kuwa Mjasiriamali lazima uamue kuwa mtatua matatizo kwenye jamii uliyopo. Hii ni kanuni ya kwanza kabisa, popote unapokuwa lazima ukumbuke kuwa wewe upo kwa ajili ya kuleta suluhisho kwenye jamii yako. Watu wenye mafanikio makubwa duniani ukiangalia mwanzo wao wameanza kwa kurahisisha matatizo ya watu.

Kila fursa inayokuja mbele yako iangalie kwa jicho la mtatua matatizo, jiulize kwa fursa hiyo unakwenda kuwasaidia vipi watu?

2.Kuwa na maono makubwa

Pamoja na kuwa mtu unaeweza kuona fursa kwenye kila tatizo linalokuja mbele yako lazima uweze kuwa na maono. Maono ndio yatakuwa msaada wako wa kufika mbali. Pasipo ya maono unaweza kujikuta umekuwa mtu wa fursa tu. Kila linalokuja mbele yako unafanya bila kuelewa linakupeleka wapi.

Wajasiriamali ni watu wenye maono na sio wapiga dili, yaani wale wanaotazama tu sehemu ya kupiga pesa za haraka haraka kisha wapotee.

Maono yako yanapaswa yawe juu yako binafsi na juu ya kile unachotaka kuleta mabadiliko kwenye dunia hii. Ni lazima ujenge maono makubwa kwasababu tayari tuna watu ambao ni mfano kwetu waliofika mbali sana.

Usiogope kutengeneza maono makubwa kwenye kile unachokifanya.

3.Kuwa na Vipambele.

Ukiwa na maono unakuwa na nafasi nzuri ya kufanyia kazi kanuni hii ya vipaumbele. Mjasiriamali anaetaka kufika mbali lazima awe amejiwekea vipaumbele vyake. Kutokana na maono yake lazima ajue anapaswa kufanya nini na vitu gani hapaswi kufanya kabisa.

Kuna nyakati zinaweza kuja dili nyingi za pesa kama ukiwa sio mtu wa vipaumbele utajikuta unapoteza mwelekeo au wakati mwingine kuingia kwenye kutapeliwa.

Tambua thamani yako,

Tambua uwezo ulionao.

4.Mfahamu Mteja wako

Unapoamua kuwa mtatua matatizo lazima ukubali kuwafahamu hao unaowatatulia matatizo yao. Hapa haina maana uwajue kwa majina hapana. Unatakiwa ujue tatizo unalotatua linawakabili watu wa aina gani.

Je ni watoto?

Wanafunzi?

Wafanyakazi?

Ni wazee?

Uwezo wao wa kipato ni upi?

Hii itakusaidia ujue hata wakati unapanga bei unaweza kupanga kulingana na uwezo wao wa kipato na mazingira waliyopo. Huwezi kusema wewe ni Mjasiriamali halafu hufahamu bidhaa yako inatumika na watu wa aina gani Zaidi.

5.Siku Zote Bidhaa zako Zitimize Mahitaji ya Wateja.

Mfano wewe unauza nguo, na mara nyingi wateja wako wakija kununua nguo zinakuwa haziwatoshi, wewe unawaelekeza kwa fundi nguo aliepo jirani kidogo na duka lako. Siku yule fundi nguo akipata akili akaanza kuuza nguo ujue utafunga biashara.

Hapa namaanisha kwamba kama unachokiuza hakimridhishi mteja atakwenda kwa mtu mwingine anaeweza kumridhisha. Usikubali mteja aondoke ananung’unika.

Kuna watu wanasema huwezi kumridhisha mteja hata ufanye vizuri bado atalalamika. Mimi nakwambia ukiona hivo basi hujajua vizuri wateja wako. Kama kuna sehemu watu wanaambiana kwamba kunahuduma nzuri basi ujue wameridhishwa na huduma.

Kwa kupitia wateja wako kuridhika wataleta wateja wengine Zaidi na Zaidi. Usikubali kutoa huduma mbovu kwa kigezo cha wewe kunufaika.

6.Tengeneza Mpango Mzuri wa Biashara.

Kama Mjasiriamali ili uweze kutimiza maono yako makubwa lazima uwe na mpango wa biashara yako. Mpango ndio ramani ya kule unakoelekea.

Mpango ndio utavuta wawekezaji wakupe mtaji.

Mpango ndio utafanya upate watu sahihi wa kufanya nao kazi.

Utakuwa unafanya makossa makubwa kama huna mpango wa biashara yako. Ni kama mtu anaefuata njia ambayo hajui inampeleka wapi. Hata kama unajua unapokwenda kuwa na mpango ni muhimu.

Mpango wa muda mfupi na muda mrefu wa biashara yako, mwaka mmoja na kurudi hadi siku moja ni mpango mfupi. Miaka 2 na kuendelea ni mpango mrefu.

 

7.Wajibika kwa Kila Linalotokea.

Lazima uwe mtu ambaye unawajibika linapotokea tatizo kwenye baishara yako. Hutakiwi kulaumu wateja, wawekezaji, wala wafanyakazi. Chukua Hatua haraka pale inapohitajika.

Wewe ndio umebeba maono ya biashara yako lazima ukubali kubeba wajibu pale unapohitajika.

Kama mtatua matatizo lazima uweze kutatua vizuri matatizo kwenye biashara yako.

8.Chagua timu sahihi

Ili uweze kuwa na ukuaji mzuri lazima ujenge timu nzuri ya kukuwezesha kutimiza maono yako. Watu wengi wanafeli kwasababu hawajaweza kuwa na watu sahihi kwenye biashara na maono yao.

Vipo vigezo vingi vya kuangalia unapochagua watu lakini muhimu ni uwe na watu ambao wanaziba mapungufu yako. Sio unachagua watu ambao wanakuja kufanya kile ambacho wewe mwenyewe unaweza kufanya.

Pia lazima uangalie watu wenye tabia kama zako, waadilifu na waaminifu, na mwisho kabisa wawe wanaamini kwenye maono makubwa uliyonayo. Ukiwa na watu wasio kuamini utajikuta kila mara unakuwa peke yako. Maana yake ni kwamba kutakuwa na watu wanaokata tamaa njiani.

9. Wekeza Muda Kwenye Ukuaji na Masoko.

Biashara yeyote yenye mafanikio makubwa ilianza chini. Kilichofanya ifike mbali ni pale waanzilishi wake walipoamua kuwekeza muda kwenye ukuaji wa biashara hiyo.

Ili biashara ikue lazima na wewe ukubali kukua, yaani uwe unajifunza kwa bidii ili uendane na ukuaji wa biashara la sivyo itakuja kukushinda huko mbele.

Lazima ukubali kuwekeza muda kwenye masoko na mauzo. Kama huuzi maana yake biashara yako haina mzunguko. Na kama haina mzunguko inakwenda kufa.

Haijalishi una bidhaa nzuri kiasi gani lazima ujitangaze mara kwa mara. Yapo makampuni makubwa yameanzishwa miaka mingi iliyopita lakini bado kila siku utaona wanatangaza bidhaa ile ile kila siku. Hii ni kwasababu usipotangaza watu wanasahau.

10. Usiishie Njiani.

Jambo la mwisho kabisa wewe kama umeamua kuwa Mjasiriamali usikubali kuishia njiani. Usikubali kukata tamaa. Wajasiriamali wakubwa kama kina Bill Gates waliweza kufika sehemu waliyopo sasa hivi kwasababu hawakukubali kukata tamaa na kuacha yale maono yao makubwa.

Pamoja changamoto nyingi lazima ukubali kuendela kubeba maono yako. Hata kama watu watakuacha endelea kusimamia kanuni hii na usikate tamaa.

Kazi imebaki kwako kufanyia kazi Hiki ulichojifunza.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/coach

Mambo 5 Ambayo kila Mjasiriamali Anapaswa Kuwa Nayo.

Habari za leo ndugu msomaji wa makala hizi kila siku ndani ya USIISHIE NJIANI. Ni matumaini yangu unaendelea vyema na maisha yako.  Leo tunazungumzia mambo ambayo kila mjasiriamali anapaswa kua nayo ili aweze kufanikisha kile anachokifanya. Tujifunze pamoja.

1. Mbunifu

Mjasiriamali yeyote kama unataka kua wa tofauti na wenzako na kuleta thamani kwa mteja wako unapaswa kua mbunifu.

Jaribu kuifahamu vyema biashara yako ili uweze kubuni njia mbali mbali za kuikuza.

Fahamu ni nini hasa mteja anataka kutoka kwako na ujue jinsi ya kumpatia kwa ubora wa hali ya juu ili asiweze kwenda kwa mwingine.

Sasa hivi tupo kwenye Information Age. Kizazi cha taarifa kila kitu siku hizi ni mtandao jaribu kubuni njia za kuwafikia wateja wako sehemu walipo kwa urahisi zaidi.

Kua mbunifu kwenye namna unavyotangaza biashara yako siku hizi mambo yamekua ni rahisi sana.

2. Mvumilivu

Mjasiriamali yeyote ambaye hana uvumilivu huwezi kumuita ni mjasiriamali. Lazima utambue kwamba umeingia katika sekta ambayo utapitia mambo magumu ya aina mbali mbali. Kwenye ujasiriamali unakwenda kujenga biashara yako kubwa mwenyewe hivyo wakati mwingine wengine hawatajua unachokipigania wata kuacha mwenyewe Inawezekana ni mke wako au hata mume, ndugu jamaa na marafiki wanaweza kukukimbia vumilia maana wao hawajui kile unachokipigania,  hawajui kile unachotaka kujijenga.

Inawezekana umeanzisha biashara ikafa bado haimaanishi ujasiriamali umeisha vumilia na anza tena.

Uvumilivu utaletwa zaidi na kile unachokitaka kwenye maisha yako. Ni ndoto gani uliyonayo unataka kuitimiza kwa kupitia unachokifanya?  Hiyo ndoto ndio ikufanye wewe uweze kua na Uvumilivu hata wakati ule umeanguka. Umekataliwa au umeachwa.

3. Mthubutu

Mjasiriamali lazima uwe mthubutu. Usiogope kuchukua hatua kama kuna kitu Umeona kinaweza kukuza kubadili biashara yako kifanye bila kuogopa. Kama umepata wazo jipya lifanye bila kuogopa.  Usiogope watu watasema nini juu yako. Maana hata wakisema bado wewe ndio una shida zako na unatakiwa uweze kuzitatua. Thubutu kwenda mbele hatua nyingine zaidi. Thubutu kufanya mabadiliko kwenye biashara yako.

Thubutu kua mbunifu.

4. Anaejifunza kupitia changamoto.

Kama umechagua kua Mjasiriamali unatakiwa utambue kwamba changamoto ni kitu ambacho huwezi kukikwepa. Huwezi kukwepa changamoto.

Changamoto ndio zinakufanya wewe ukomae.

Changamoto zinakujengea msingi mzuri wa biashara yako na wewe binafsi.

Ili uweze kuja kua mtu mkuu hapo baadae lazima ukubali kupitia changamoto nyingi.

Usiwaone matajiri wakubwa kama kina Mengi, Bakhresa na wengineo wamesimama kwenye utajiri wao muda mrefu bila kuyumba ukafikiri ni uchawi. Walikopitia ndio pamewajengea msingi imara na hata sasa unawaona wamesimama. Chukulia changamoto kama ni shule yako jifunze na mwisho wako utakua mzuri.  Unapopitia changamoto usilalamike wa kulaumu.

Kesho yako inakwenda kua bora.

5. Mwenye Maono.

Mjasiriamali lazima uwe na maono. Maono ninayozungumzia mimi ni makubwa. Hapo kwenye ukubwa tunatofautiana vipimo sasa wewe pima mwenyewe kisha uyatambue vyema maono yako. Kwa kifupi ni kwamba kwenye biashara yako unataka uifikishe wapi? Miaka kumi au ishirini ijayo unataka mtaji wako ufikie kiasi gani?  Miaka kumi ijayo unataka biashara yako ienee hadi wapi? Miaka mitano ijayo unataka uajiri wafanyakazi wangapi? Hivyo ni vitu vya msingi unatakiwa uwe navyo kama mjasiriamali. Maono ni kitu cha muhimu maana yanakupa mwelekeo wa biashara yako na mwelekeo wako binafsi huwezi kuyumbishwa na vitu vinavyotokea kama una maono.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Vinavyowezekana na Visivyowezekana.

Mara nyingi tunapenda Zaidi kufanya yale ambayo yanawezekana kwenye uwezo wetu wa akili. Sio vibaya lakini unakuwa hakuna cha tofauti ambacho utakipata.

Watu wote ambao wameweza kugundua mambo makubwa na yakaleta mapinduzi kwenye dunia na kwenye Maisha yao walijaribu yale ambayo yalionekana kama hayawezekani kabisa.

Vile vyote ambavyo vinawezekana vinakufanya wewe uwe sawa na wengine wote. Wewe kama mjasiarimali unapaswa kujua kwamba kama unataka kuleta mabadiliko makubwa kwenye unachokifanya kubali kujaribu yale ambayo yanaonekana hayawezekanagi.

Kuna mambo ambayo wamesema kwamba watu wengi wamejaribu wakashindwa basi hiyo ndio sehemu yako ya kutokea. Ukiweza kufikiri vyema na Zaidi ya wengine utagundua namna ya kutatua kile kilichoshindikana.

Unapochukua Hatua ndogo ndogo kwenye vile vitu vinavyoonekana ni vigumu unakuwa unaijenga akili yako na kuifanya iamini juu ya uwezekano.

Kama Mjasiriamali ni lazima ujue kwamba wewe kukua ni lazima, kile ulichokianzisha kisiishie kuwa kama wengine ambao walishafanyaga. Hili litawezekana pale ambapo utaamua kujaribu vile vitu ambavyo vinaonekana kama hakuna uwezekano.

Lazima ukubali kuwa na nguvu ya uthubutu wa kuchukua Hatua kwenye vile vitu ambavyo vinaonekana haiviwezekani.

Lazima uwe na Imani ili uweze kupata nguvu ya kuchukua Hatua bila ya kusita sita. Imani yako ndio inakuamulia nguvu ya kuchukua Hatua.

Usikubali ukomo aliojiwekea mtu mwingine ukawa ni ukomo wako wewe. Amini inawezekana na chukua Hatua.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Jacob Mushi,

Author | Trainer | Entrepreneur

Simu: 0654 726 668 |0755192418,

Twitter:  @jacobmushitz

Instagram: @jacobmushi

Facebook:  Jacob Mushi 

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

KAMA UNA SIFA HIZI WEWE NI MJASIRIAMALI

Habari za leo mwanamafanikio. Leo ninataka kukuonyesha mambo machache ambayo yanaonyesha wewe ni Mjasiriamali. Katika dunia ya sasa tunahitaji watu wengi ambao ni wajasiriamali watu ambao wako tayari kuchukua hatua kubadilisha Maisha ya wengine pamoja na ya kwao wenyewe.

1.Decision maker (Mfanya Maamuzi)

Kama wewe una uwezo wa kufanya maamuzi linapotokea jambo mbele yako bila kusita una sifa ya Mjasiriamali. Unapokutana na fursa Fulani nzuri unaweza kuitazama na kuamua moja kwa moja bila kutegemea ushauri wa watu wengine. Nimekuja kugundua kwamba tuna watu wengi sana wanaoshindwa kufanya maamuzi hadi wasikie wenzao wanasemaje. Kama wewe bado una tabia hii una safari ndefu sana ya kufikia mafanikio yako. Kama unakutana na fursa halafu ili ukubali hadi ukamuulize mwenzako mimi nakuhurumia. Na hii inatokana na uvivu wa kusoma na kutokuzijua taarifa za vitu mbalimbali. Hivyi unapokutana na kitu kipya unakuwa na mashaka ya kuamua. Mjasiriamali ana uwezo wa kutoa maamuzi na siku zote anakua na majibu matatu la kwanza ni NDIO, HAPANA, NALIFANYIA UTAFITI NITAKUJIBU BAADA YA MUDA FULANI. Kama wewe huwezi kuwa na majibu hayo na ukayasimamia huna sifa ya mjasirimali. Wengi wetu tukisema ndio hatumaanishi ndio tunasema ndio ili kumridhisha anaetuelezea wazo.

2.Risk taker (Asiogopa Hatari)

Mjasiriamali ni yule asiyeogopa hatari yeye wakati mwingine yupo tayari kuweka mtaji wake kwenye biashara ambayo hajawahi kuifanya lakini anaamini itamfikisha kwenye maono yake. Yupo tayari kwenda sehemu ambayo hajawahi kufika ili akaanzishe biashara mpya huko. Yupo tayari kuvumilia misukosuko yote anayoipata kipindi biashara inapoyumba au anapopata hasara. Yupo tayari kurudia biashara aliyofanya akashindwa.

Wewe umejaribu hatari ipi mpaka sasa ili tukuite Mjasiriamali? Umejaribu njia gani ya kufikia ndoto zako? Kama bado basi wewe sio Mjasiriamali. Kama unaogopa kupoteza pesa yako kidogo kwenye biashara ambayo hujawahi kuifanya au ni ngeni basi wewe huna sifa hiyo ya Mjasiriamali. Anza sasa kufanya na kujiingiza kwenye vitu ambavyo hujawahi kujaribu.

SOMA: USIYOYAJUA KUHUSU PESA HAYA HAPA

3. Self-confidence (Anaejiamini)

Mjasiriamali anajiamini kwa kile anachokifanya. Ana uwezo wa kuelezea vyema bidhaa yake bila kuogopa. Anajua anachokifanya na anapokwenda hivyo hana wasiwasi wa kushindwa au pale anapokosea. Jijengee sifa hii ya kujiamini na wewe utakaribia kuwa Mjasiriamali.

4. Leader (KIONGOZI)

Mjasiriamali yeyote ana sifa ya kiongozi kwasababu ameweza kujiongoza mwenyewe na anakwenda kuongoza biashara zake mwenyewe. Kama huna sifa ya kiongozi lazima utapoteza biashara zako pamoja na watu uliowaajiri. Kama huna sifa ya uongozi huwezi kufikisha maono yako mbali itakubidi uje uweke watu wenye maono makubwa Zaidi yako. Uongozi unaanza kwa kuweza kujiongoza mwenyewe.

5. Problem Solver (Mtatua Matatizo)

Ni mtu anaetatua matatizo ya watu popote anapokwenda huangalia watu wanapitia shida gani, ndipo huwaletea suluhisho na kutengeneza kipato. Kama wewe huwezi kuyaona matatizo ya watu kwenye jamii ni ngumu sana kuleta suluhisho. Hakikisha kila unapokwenda unatazama kwa jicho la tatu. Angalia ni kwa namna gani unaweza kuwasaidia wengine na wewe utengeneze kipato.

Matatizo yapo kila kona ndio maana watu hua wanashinda wakilalamika. Watu wenye sifa hii ya ujasiriamali huona tatizo haraka na kuleta suluhisho.

6. Vision (Mwenye Maono)

Ni mtu mwenye maono. Anaona mbali sana. Sio mtu anaefanya biashara ilia pate faida ya leo pekee. Lazima awe na maono ya kufikisha mbali wazo lake ili kuacha alama kwenye jamii inayomzunguka. Je wewe una maono? Unajua kuandika maono yako? Umeshaanza kuishi maono yako? Unachokifanya leo kinagusa nini kwenye maono yako?

Tunahitaji wajasiriamali wengi sana ili kuweza kutatua matatizo mengi yanayolikumba bara la Afrika. Unaweza kuwa mmoja wao.

Jacob Mushi,

www.jacobmushi.com/coach

JINSI YA KUPATA WAZO LA BIASHARA

Habari rafiki, leo nataka nikuonyeshe njia mbalimbali za kupata wazo la biashara na mtaji. Inawezekana mwaka huu una mpango wa kwenda kuanza biashara yako mpya Makala hii itakua msaada kwako. Inawezekana pia una wazo la biashara lakini hujui utatoa wapi mtaji Makala hii pia itakwenda kukuonyesha mwanga.

Njia za kupata WAZO LA BIASHARA:

 •  Find something that add value to the life of others. (Kitu kinachoOngeza Thamani kwenye Maisha)

Ni kitu gani kinaongeza thamani kwenye Maisha ya wengine? Ni kitu gani ukikifanya hapo ulipo utafanya watu wafurahie Maisha yao? Ni kitu gani kitafanya Maisha ya watu unaowafahamu yawe marahisi? Ukiweza kujua vitu hivyo hapo utakuwa umepata wazo la biashara na unaweza kuanza na kufikia mafanikio makubwa sana. Kama unataka wazo lako lidumu hakikisha unachagua kitu ambacho watu wataendelea kukihitaji kwa muda mrefu sana. Mfano labda ni vocha zinapatikana kwa shida ukiamua kuwapelekea vocha hakuna siku shida yao ya vocha itakwisha. Lakini ukiwauzia masweta ya kupunguza baridi ujue kuna kipindi cha joto hawatahitaji masweta au wanaweza wakatunza masweta yao mwisho wateja wakapungua. Mtu aliegundua internet na anaemiliki mitandao ya simu hawa ni watu ambao biashara zao zitadumu kwa muda mrefu sana duniani hadi pale mapinduzi mengine ya teknolojia yatakapokuja. Embu jiulize ni tatizo gani la kujirudia rudia lipo kwenye jamii yako ulete suluhisho Maisha ya wetu yawe bora.

SOMA: JINSI YA KUZISHINDA CHANGAMOTO KWENYE BIASHARA NA UJASIRIAMALI

 • Find a Solution to the problems (Tafuta suluhisho kwenye matatizo)

Kwenye matatizo kuna aina mbalimbali ya matatizo kwenye jamii. Unaweza kuangalia ni tatizo gani kubwa linaikumba jamii yako ukatafuta suluhisho na ikawa ni biashara yako kubwa sana. Kamwe hata siku moja usiweke faida mbele kwenye kutatua matatizo ya watu. Wateja wako watakukimbia. Ndio unahitaji faida sana lakini ongeza bidii Zaidi kwenye utatuzi wa tatizo. Wengi wetu hujisahau mwanzoni unaanza vizuri ukishapata pesa kidogo unaanza kusahau kama upo pale kutatua matatizo ya watu. Watu wana matatizo mengi sana kwenye jamii zetu angalia ni aina gani ya tatizo unaloweza kuliletea suluhisho kisha ulikuze iwe ni biashara yako.

 •  Do what you love (talents and hobbies) (Kipaji au kitu Unachopenda kufanya)

Una kipaji? Unapendelea kufanya kitu Fulani Zaidi? Je unajua kwamba unaweza kugeuza kipaji chako au unachopenda kuwa wazo la biashara? Mfano unapenda kuchora, unaweza kuchora kwa biashara. Unaweza kuwachora watu ukawapa wakakulipa. Unapenda kutunga hadithi? Unaweza kuandika hadithi zako ukaziuza ua ukaziweka mtandaoni watu wakasoma baada ya muda ukaweka gharama ya kulipia ili wasome hadithi zako. Au ukaandaa vitabu vya hadithi zako ukauza. Karibu kila ulichonacho unaweza kukigeuza kuwa wazo la biashara. Kasoro kuuza mwili wako au kulala. Kama bado hujajua una kipaji gani au unachokipenda utakigeuzaje kuwa wazo la biashara wasiliana nami kwa ushauri Zaidi.

SOMA: KAMA UNASIFA HIZI WEWE NI MJASIRIAMALI

 •  Skills and experiences (Ujuzi na Uzoefu)

Una ujuzi wowote au uzoefu katika jambo Fulani? Unaweza kutumia hiyo kama wazo lako la biashara na ukajiajiri. Tuchukulie mfano wewe umesomea IT (Information Technology) halafu unaweza Zaidi kutengeneza Website au kutengeneza matangazo ya picha. Hilo tu linatosha wewe kuanza kama biashara yako na ukaikuza taratibu hadi ikafikia kuwa biashara kubwa sana. Tatizo la wengi hawataki kupata hasara, hawataki kuanzia chini, hawataki kufanya kazi kwa bidii na ubunifu. Mtu anataka aanze leo halafu kesho apate idadi ya wateja anaowataka. Hiyo haiwezekani kirahisi hivyo labda utumie jina la mtu. Kubali kuumia, vumilia na mwisho wake utaona matunda ya jasho lako.

 • People’s needs (Mahitaji ya Watu)

Watu wanahitaji nini kwenye jamii yako? Kwa mfano ukiona watu wengi wanakimbilia kwenye kilimo badala na wewe kukimbilia kulima unaweza kuwauzia mbegu, au ukawapa elimu bora juu ya kilimo wanacholima. Inawezekana unafahamu vitu vingi sana kichwani kwako na watu wanavihitaji hadi sasa hujajua kama unaweza kutumia hiyo kama biashara yako? Jaribu kuitazama jjamii uliyonayo kisha utagundua inahitaji nini na wewe una kitu gani ambacho unaweza kuipatia. Hivi sasa tuna vijana wengi ambao wamemaliza chuo na hawana ajira. Kitu cha kushangaza sana ni pale mtu anaposhindwa kuwaza ataitumiaje elimu aliyoinayo atengeneze kipato. Kama uliweza kwenda kusomea kitu chuoni miaka 3 halafu leo unakaa nyumbani mwaka mzima huna cha kufanya huoni ulikuwa unapoteza muda?  Jaribu leo kutafakari unawezaje kuutumia ujuzi au elimu uliyonayo kujiajiri au kama wazo la biashara. Kama bosi wako angekutumia wewe ili akulipe kwanini unashindwa kufikiri ni kwa namna gani ujitumie ujilipe?

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

MAMBO 5 NILIYOJIFUNZA LEO -4

Habari rafiki,  unaendeleaje.  Leo tena tunakutana na mambo haya matano niliyojifunza siku ya Leo. Karibu sana rafiki yangu tujifunze pamoja.

1. Uaminifu ndio Mtaji Wako.

Hakuna binadamu mwingine atakaependa kufanya kitu chochote na wewe kama huna uaminifu.  Hakuna atakaependa kuwa na wewe kwenye mahusiano. Hakuna atakaependa kufanya biashara na wewe. Hakuna atakaependa kukupa kazi.

Kabla hujaingia kwenye biashara au jambo lolote linalohisisha binadamu wenzako anza na uaminifu.

Uaminifu ni kutekeleza yale unayoaihidi, kusimama imara kwenye kile unachoamini bila kuyumbishwa.  Kutokusema uongo ili upate kitu fulani au uonekane mwema.

Kuwa mwaminifu kwenye mambo yote ndugu yangu.

2. Bidii Yako Ndio Itaamua Uende wapi.

Fanya kazi kwa bidii,  kuwa na uaminifu peke yake haitoshi lazima uende hatua nyingine ya kufanya kazi kwa bidii. Hii itaongeza sifa yako ambayo itaaamua watu wapende kufanya kazi na wewe.

“Huyu mtu ni mwaminifu na mchapakazi.” Bidii yako itafungua milango ya fursa mbele yako.  Katika kufanya kazi ndio utakutana na watu ambao watakupa mawazo ya maendeleo.

Kumbuka usiingie kwenye kufanya kwa bidii kama huna uaminifu utadondoka njiani hutafika popote.

3. Tatizo lolote Unaloliacha Unalifanya Liwe kubwa zaidi.

Tatizo unalopitia kama hutalitafutia ufumbuzi linaongezeka ukubwa. Kama tatizo ni kwenye mahusiano yako na unalifumbia macho au unajifanya kama hakuna tatizo ujue ipo siku litakuwa baya zaidi. Hii ni kwasababu mmoja wapo akichoka atakwenda kutafuta suluhisho kwingine.

Tatua matatizo au changamoto unazokutana nazo ukiziacha zitazidi kuwa kubwa. Ongeza uwezo wako wa kuelewa na kutatua matatizo makubwa zaidi.

4. Kadiri Unavyokua Ndio Changamoto zinaongezeka.

Kama jana ulikuwa hatua fulani ya maisha ukafanikiwa kusogea mbele, unakuwa umekaribisha changamoto nyingine zaidi. Unapongezeka unaongeza matatizo.

Mfano wewe una biashara yako,  imekua kiasi ulikuwa mwenyewe sasa hivi umeajiri watu watano. Hapo ujue umeongeza changamoto kwenye biashara maana kila mtu anakuja na tabia zake,  mwingine atakuwa mvivu, mwingine sio mwaminifu. Hivyo akili yako itafanya kazi zaidi kwenye kuwaangalia watu ulioajiri na bado biashara Imekuwa kubwa zaidi.

Umeoa mmeongezeka matatizo nayo yanaongezeka kama wewe ulikuwa na tabia zako fulani fulani hivi ujue na mwenzako atakua nazo.

Kila hatua unayosogea ina changamoto zaidi. Lakini ni vibaya sana kubakia sehemu ile uliyopo kwani ni matatizo zaidi ya unavyofikiri.

5. Kitu gani Mtu akikigusa kwako anagusa maisha yako?

Kila mmmoja ana sehemu ambayo hataki mtu alete mchezo kabisa. Sehemu ambayo ukikuta mtu anafanyia mzaha basi unaweza kugombana nae hata kama hujui kugombana.

Inawezekana ndio kitu ulichokipigania muda mrefu hadi kikasimama. Inawezekana ni mtu unayempenda sana.

Kila binadamu ana kitu ambacho hayupo tayari kuona mtu anakifanyia mzaha au kukipoteza.

Wewe umeshafahamu ni kitu gani?  Hakikisha unakifahamu mapema.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

JINSI YA KUZISHINDA CHANGAMOTO UNAZOKUTANA NAZO KWENYE UJASIRIAMALI NA BIASHARA.

Habari za leo Mwanamafanikio mwenzangu. Najua una pilikapilika nyingi kipindi hiki cha siku kuu. Lakini mimi pia bado nipo kwa ajili yako. Hivi unajua kwamba kipindi hiki watu ndio wananunua Zaidi? Kama ni hivyo basi wauzaji wananufaika sana. Je wewe umefanikiwa Kuuza chochote siku kuu hizi? Kama hujafanikiwa basi mwaka 2017 usikupite hivi hivi jipange tu ni kitu gani ungependa watu wanunue kutoka kwako vipindi vyote vya siku kuu.

Karibu kwenye Makala yetu ya leo tunazungumzia ni namna gani unaweza kushinda changamoto unazopitia kwenye ujasiriamali na biashara. Ni mambo ya muhimu sana ukiweza kuyafanyia kazi yote utafanikiwa. Usiogope changamoto kwani ndio zinatufanya tupande viwango. Matatizo au changamoto unazoziogopa leo na kuziruka zitakuja kukukwamisha huko mbeleni. Yaani kama sasa hivi ulitakiwa ujifunze kitu Fulani ukazembea ipo siku utatakiwa kutumia kile ulichotakiwa kujifunza na kwa kuwa uliruka basi utahitaji gharama kubwa Zaidi au ukose fursa iliyopo mbele yako.

 •  Never Give Up (Usikate Tamaa)

Kama umeamua kabisa kwamba utafanya hadi ufikie ndoto na maono yako usikubali kukata tamaa pale unapopitia changamoto. Jitie nguvu ili uweze kusonga mbele. Tafuta au namna ya kutatua tatizo sio kulikimbia. Safari ya mafanikio ni sawa na ile safari ya wana wa Israel kwenda Kaanani. Ukisema ukate tamaa urudi utarudi peke yako wenzako tunasonga mbele. Na ukisema ubaki hapo ulipo hutaweza kuishi kwani ni jangwani hivyo kuna siku utakosa maji na chakula na utakufa. Hivyo pia na mafanikioa usikubali kurudi nyuma wala kubaki hapo ulipo. Songa mbele

 • Never Stop Learning (Usiache Kujifunza)

Kamwe usiache kujifunza kuna njia nyingi za kujifunza sana. Kipindi hiki teknolojia imekua kubwa namna ya kupata taarifa mbalimbali za kukusaidia kwenye kile unachokifanya imekuwa ni rahisi sana. Kusoma vitabu imekua rahisi sana. Unaweza kuingia kwenye mtandao wa YouTube kwa kupitia simu yako au computer na ukajifunza mambo mengi mno kupitia videos. Unaweza kujifunza vitu mbalimbali kwa waliofanikiwa kwa njia rahisi. Hata kupitia group za WhatsApp kama upo kwenye kundi ambalo hujifunzi chochote hakuna haja ya kukaa humo maana ni kupoteza muda na pesa. Tafuta sehemu ambayo utajifunza hata kama utalipia pesa lakini uweze kusonga mbele kwenye kile unachokifanya.

 • Don’t Afraid to Fail (USIOGOPE KUSHINDWA)

Kamwe usiogope kushindwa ipo mifano mingi ya watu walionza vitu vyao lakini wakafanya na wakashindwa. Lakini kwao haikuwa ni mwisho walijaribu tena na tena hadi wakapata matokeo. Kama umeanza biashara kwa mara ya kwanza na ukapata hasara furahi sana maana umepata kitu cha kujifunza. Kama bado hujapata hasara yeyote au changamoto ogopa sana na angalia vizuri unachofanya kwani inawezekana husogei mbele umesimama sehemu moja tu. Ukianguka Inuka anza tena. Mtoto mdogo anapojifunza kutembea akianguka sio mwisho wa kutembea. Wewe ulipokuwa shuleni ukifeli jaribio sio mwisho wa kusoma tena. Hata ukifeli mitihani ya kumaliza shule nafasi za kurudia hua zipo. Hivyo hata katika biashara yako kushindwa kusikunyime nafasi ya kufanya tena.

 • Focus on Your Goals (Lenga kwenye Malengo yako)

Hakikisha unachokifanya kinalenga malengo yako. Yapo mambo mengi sana huku duniani ambayo ukiyasikiliza yanaweza kukutoa katika kile unachokifanya hivyo kujikuta hujafanya chochote. Huku duniani kuna fursa nyingi sana zinajitokeza kila siku kama utashindwa kulenga kwenye maono na ndoto zako utajikuta unapoteza mwelekeo na kufanya kila kinachokuja mbele yako. Jifunze kusema Hapana ukiwa umemaanisha hapana na Ndio ukiwa umemaanisha Ndio. Sio kila vita ni ya kwako sio kila pambano unatakiwa kupigana. Jiulize kwanza linaleta matokeo gani kwenye baadae yangu?

 • Find a Coach (Tafuta Kocha)

Tafuta Kocha au mtu wa kukushauri kwenye changamoto unazopitia. Mtu huyu unaweza kumpata kwa gharama ya malipo au bure kutokana na unavyofahamiana nae. Ila ukweli ni kwamba ushauri wa bure wengi hatufanyii kazi nimeshashauri watu wengi lakini huwa wanaondoka tu bila kufanyia kazi wanachoshauriwa. Wengine ukiwaambia ukweli huwa wanaondoka kimya na meseji hawajibu tena. Ukiwa na Kocha ambaye unamlipa na anakushauri lazima utatendea haki pesa yako. Lazima utafanyia kazi ushauri wake. Hakuna namna nyingine ya kufikia mafanikio bila kulipa gharama.

 •  Jichanganye na Wenye Mafanikio Zaidi yako Kwenye Kile unachokifanya.

Hakikisha umezungukwa na watu wengi wanaofanya vizuri kile unachokifanya kwani kwa kupitia watu hao utaweza kujifunza mambo mengi sana kwao. Utaweza kuwashirikisha changamoto zako na ukashauriwa. Inawezekana unachopitia alishapitia mtu Fulani na akaweza kuvuka hivyo ukapata msaada.

 • Tembelea Blog Hii Kila siku

Sio utani namaanisha kweli utembelee blog hii kila siku ili uweze kujifunza mambo mbalimbali ya kukuvusha kwenye changamoto uanzopitia. Kama umeona kuna mambo umeweza kuyapata ndani ya Blog hii yakakusaidia endelea kujifunza kila siku na kadiri tunavyoendelea kuwa pamoja utapata vitu vingi Zaidi na bora kwa ajili yako.

 • Jiunge na Inuka Uangaze

Kama unataka kuwa pamoja na mimi karibu Zaidi uweze kujifunza mambo mengi Zaidi na wanamafanikio wenzako jiunge na mtandao wetu wa Inuka Uangaze kwani utaweza kupiga Hatua mbalimbali katika Maisha yako ya mafanikio. Nipo kwa ajili ya kuhakikisha unafanikiwa kwenye kile unachokifanya wewe pekee ndiye unatakiwa uwe tayari.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Jacob Mushi,

Author | Trainer | Entrepreneur

Simu: 0654 726 668 |0755192418,

Twitter:  @jacobmushitz

Instagram: @jacobmushi

Facebook:  Jacob Mushi 

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

NAMNA YA KUWEZA KUFIKIA MAFANIKIO NA BIASHARA YAKO

Habari za leo Rafiki? Ni siku nyingine tena ya Baraka sana kwangu. Natumaini na kwako ni ya baraka Pia. Tunapopata nafasi ya kuwa na nguvu ya kuendelea kufanya yale tunayafanyayo ni vyema sana kushukuru.   Mwaka ndio huoo unaanza kwenda wewe unaelekea wapi? Leo ni tarehe 9 siku tisa zimeshapita wewe umeshaanza kuacha alama gani kwenye hizi siku tisa za mwaka huu? Yaani ndio hivyo mwaka unaishaga ni sekunde moja inacheza na kutengeneza dakika na dakika nayo inakwenda hadi masaa 24.

Kunakuwa asubuhi, mchana, jioni na hatimaye usiku siku inapita. Hivyo ukidhani kuna kitu cha tofauti kwenye mwaka mpya utakuwa unakosea. Utofauti wa mwaka unaweza kuwa ni majira tu hasa vipindi vya mvua na jua. Jua linaweza kuwaka sana ua mvua ikanyesha sana hayo ndio mambo yanayoweza kuwa mapya.    Maisha yako yatakuwa mapya kama wewe mwenyewe utaamua kubadilisha vile vitu ambavyo unavifanyaga kila siku. Na vitu hivi vinabadilishwa kwa kubadili fikra zako. Ukibadili unavyofanya kila siku utabadili matokeo yako. Utatengeneza mfumo mzuri wa Maisha ambao utakuletea matokeo bora Zaidi kwenye kila sehemu ya Maisha yako.   Tuachane na hilo tuje kwenye mada husika ya leo.

Tunazungumzia jinsi gani ambavyo unaweza kufikia mafanikio unapoanza na biashara ikiwa ndogo kabisa. Hapa watafiti wanasema biashara nyingi ndogo hufa sana mara nyingi baada ya kuanzishwa. Hivyo ni muhimu ukajifunza vyema somo hili ili ujue ni namna gani utaweza kuepuka kufa kwa biashara yako.  

 “Wealth is largely a result of habit.” Jack Astor Utajiri ni Matokeo makubwa ya tabia – Jack Astor   

Kama unataka kufikia mafanikio kwenye biashara uliyoianzisha jua ni tabia gani unazotakiwa uzitengeneze na kuzifanyia kazi kila siku hadi zikuletee matokeo ya mafanikio makubwa au utajiri.    

u Start Again (Anza/Rudia tena)

Haijalishi umeshindwa mara ngapi haimaanishi ndio mwisho. Bado ukisema uache kufanya biashara Maisha hayatakuwa marahisi. Hakikisha unaivuka changamoto hii ya kushindwa na kuacha. Hapo unapoachia ndipo sehemu itakuwa inakusumbua kila wakati na hata ukifanya kingine hutaweza kuendelea mbele utakwamia pale pale ulipokwamia kwenye biashara ya mwanzo.   Kitu cha kufanya hakikisha umeweza kulitambua vyema tatizo la kushindwa kwako liko wapi. Halafu hakikisha umejua ni nani huyo anaesababisha hilo tatizo. Mara nyingi 90% mchangiaji mkubwa wa matatizo kwenye biashara yako ni wewe mwenyewe. Malizia kwa kutafuta suluhisho, utavukaje hapo ulipokwama? Kama shida ni madeni yamekuwa mengi basi tafuta suluhisho. Kama hakuna wateja tafuta suluhisho, kama ni kingine chochote tafuta suluhisho. Hakuna tatizo lisilokuwa na suluhisho. Ukipata suluhisho hakikisha unaitumia vyema uvuke hapo. Uendelee na safari yako ya mafanikio.  Rudia, Rudia Rudia Tena  

u Learn through mistakes (Jifunze Kupita Makosa Yako)

Ili kutofanya makosa ya kujirudia hakikisha unajifunza. Kila changamoto unayoipitia hakikisha unapata somo ambalo halitafanya urudie tena kosa. Siku zote naamini mtu anapovuka changamoto Fulani kwenye Maisha anakuwa mtu wa tofauti anabadilika anapanda viwango. Mfano: (Huwa nawashangaa sana wale watu wanakata tamaa kabisa kwenye mahusiano wanapoachwa au kutendwa. Ni kweli moyo unauma lakini lazima ujue kwamba kwa hilo ulilopitia hutakiwi uwe mtu wa kawaida kwasababu ni changamoto umeivuka. Imekufumbua macho ukajua kumbe kuna haya natakiwa niwe makini Zaidi. Sasa wewe ukisema haya mapenzi sitaki tena. Utakuwa unakosea sana maana huku duniani haupo mwenyewe. Kama umeumizwa tumia nafasi hiyo kuwa mtu bora Zaidi usiwe tena legelege. Jua udhaifu wako uko wapi. Jifunze jifunze jifunze. Hata ukiwa na mwingine hauwi tena mtu wa kawaida. Ukiishia kuwachukia watu na kuona sijui hawafai utateseka tu bure maana hata hawajali kwanza hawajakuumiza wao. Mara zote ninapokutana na mtu ameachwa hua napenda kujua amejifunza nini kupitia changamoto hiyo. Na siku zote huwa na mwambia usije kusema ndo mwisho sitopenda tena maana bado upo duniani na haushi peke yako huku duniani. Jifunze jua makosa yako wapi. Wewe unahusikaje katika tatizo. Kuwa makini kosa lisijirudie tena. Hata kama utaumizwa tena isiwe kwa changamoto ile ile kwasababu ulishajifunza.) Hivyo kwenye biashara waweza kutumia mfano huo kujifunza kwa makosa yako.    

u Be Persistent (Kuwa Sugu/endelea Kufanya)

Energy flows to where the concentration goes. Nguvu siku zote huelekea sehemu ili unapoweka mkazo wa kufanya. Kama una mambo kumi unafanya kuna moja utakuta unalifanya vizuri Zaidi kwasababu ndio unalipa mkazo Zaidi. Ili uweze kuwa mtu wa kufanya mambo kwa muendelezo ni muhimu sana ukaifahamu biashara yako kwa undani Zaidi. Ifahamu kuliko mtu yeyote. Hii itakupa nafasi ya kuifanya vizuri. Hujawahi kuona mama akiona mtoto analia tu ameshajua tatizo ni nini? Mtoto hawezi kusema lakini kwa vile mama anamfahamu mwanawe vyema anajua huyu ni tumbo linamuuma. Na biashara yako unatakiwa uielewa kwa kiwango cha juu sana ili linapotokea tatizo lolote uweze kulitatua mapema kabla halijawa kubwa na kuja kukushinda.  

  u Be positive (Kuwa Chanya)

Matatizo unayopitia unatakiwa uyafikiria katika mtazamo chanya. Ukifkiri kwa mtazamo hasi ndio yataharibu ile nia yako. Yatakufanya uchoke. Akili chanya siku zote huleta matokeo chanya. Kila unalopitia lipo kwasababu maalumu. Na sababu hiyo ni njema sana. Kuwa chanya kwenye kila linalokuja ili uweze pia kuishi kwa furaha.  

u Build a support network (Tengeneza Timu ambayo Intakusaidia)

Katika maisha tuna marafiki na watu wa aina mbalimbali. Kuna watu waliotuzidi vipato na umri pia. Hawa ni watu ambao unatakiwa ukae nao vyema ili uweze kupata msaada pale yanapotokea mambo magumu. Tafuta watu waliokuzidi kwenye kile unachokifanya. Tafuta watu wanaofanya kama wewe ambao mnaweza kushauriana. Mfano mdogo: wewe ni mwimbaji wa nyimbo halafu una marafiki wa karibu ambao sio waimbaji kabisa. Hawajui chochote kwenye uimbaji wao wanapenda tu kusikiliza nyimbo. Ukitoa wimbo halafu ukawatumia kwanza wasikilize wakupe maoni wanaweza wakausifia wimbo tu maana hawajui chochote juu ya wimbo. Lakini ukimtumia mwimbaji mwenzako akausikiliza anaweza kukushauri mengi. Atakwambia hili neon ungetamka hivi. Huu mziki umekuwa mkubwa sana. Na mengine mengi ambayo wale marafiki wasio waimbaji wasingeweza kujua. Maana yangu hapa ni lazima uwe na watu aina zote wanaokushauri na wanaopokea kile unachotoa. Ukiwa na wapokeaji tu unaweza kukosea na wasijue Na wewe pia usijue kama umekosea. Kila mtu ana sehemu yake kwenye Maisha yako. Tengeneza mtandao wa watu ambao ukikwama watakuwa pembeni yako.  

TAFUTA KIONGOZI.

Huyu ni Mtu ambaye atakuwa karibu yako na utakuwa unampa taarifa zako zote za biashara unazofanya. Kuna tabia ni ngumu sana kuacha bila kusimamiwa. Mfano tabia ya kuweka akiba na kuwekeza. Kubali kuwa chini, kubali kuwa mwanafunzi ufundishike ndio utafikia mafanikio. Nimesoma vitabu vingi katika vitabu unakutana na mwandishi anasema aliongozwa na mtu Fulani akafikia mafanikio aliyonayo. Sasa wewe ni nani usioongozwa? Mimi hapa nakuandikia lakini nina mtu anaenifuatilia na kunishauri. Nikipitia changamoto ananishauri kwa kila hatua ninayopiga. Tatizo kubwa tulilonalo tuna watu wengi wanaodhani wanajua kila kitu wanafikiri labda wao wanaweza wenyewe. Kama ingekuwa rahisi hivyo kusingekuwa na vitabu vya kusoma ili ugundue maarifa na kuyatumia.  

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”