HATUA YA 267: Nipo Hapa tangu 96!

Siku moja nikiwa maeneo ya stand nikakutana na watu wawili wakigombania Tsh elfu mbili mmoja katika hasira sana akamwambia mwenzake wewe mbona unakuwa kama umekuja stand jana? Kwa hasira sana mwenzake akajibu kwamba nipo hapa tangu mwaka 96 nikashangaa sana kuona watu sh elfu mbili inawafanya wajivunie kuwepo kwenye kitu kile kile bila ya mabadiliko […]

HATUA YA 266: Hili Ndio Bomu Unalojitengenezea Kila Siku.

Katika Maisha vipo vitu vingi tunafanya mara nyingi ni kwa kuiga yale ambayo wengine wanafanya, mengine tunaangalia tangu zamani walikuwa wanafanya na mengine ni asili yetu yaani unafanya kwasababu ndio asili ya kila kiumbe hai. Shida inakuja kuwa kubwa sana pale unapokuwa unafanya jambo kwasababu watu wengine wanafanya. Hapa ndipo unakuwa unajitengenezea bomu kubwa sana […]

HATUA YA 265: Mambo Yakufanya Ili Kuacha Tabia Mbaya yeyote.

Yafanya wasiwe na maisha bora na mojawapo ya hayo mambo ni tabia mbaya. Tabia hizi nyingi zimekuwa ni tatizo kwenye maisha ya watu kwani kuziacha imekuwa ni tatizo sana. Tabia nyingi mbaya huanza kujengeka kidogo kidogo na mwisho wake zinakuwa ni kama ulevi kwenye maisha yetu. Ni hatari sana kama utashindwa kufanya namna kuziacha kwani […]

HATUA YA 264: Unakuwa Kile Unachoamini.

Unakuwa Kile unachokiamini, kuamini kunakuja kwa kupitia njia mbalimbali kwanza ni kusikia, kuona, na wakati mwingine kusoma. Tukianza na kusikia kama akili yako na ufahamu wako utakuwa umeupa nafasi ya kusikia mambo mazuri yanayoendelea utajenga Imani ya mambo mazuri. Kama utaipa nafasi ya kusikia mambo mabaya yanayoendelea utajenga Imani ya kwamba kuna hali mbaya sana […]

HATUA YA 263: Vile Usivyotaka Kuonekana.

Kuna aina Fulani ya maisha ambayo mara nyingi unapenda watu wajue kuwa unayo au unayaishi lakini katika uhalisia hauishi maisha hayo. Ni kwekli sio sawa kuonyesha kila kitu wazi kwenye dunia lakini ni vyema sana yale maisha ambayo unataka watu waone na wajue kuwa unayaishi ukaanza kuyaishi kiuhalisia badala ya kujifanya. Ukiendelea kujifanya kuwa una […]

BARUA MAALUMU KWA VIJANA AMBAO BADO HAWAJAOA AU KUOLEWA.

Habari za leo Rafiki, ni matumaini yangu kila mmoja anaendelea vyema kwenye Maisha yake na kupambana ili kupata matokeo bora Zaidi. Nina Imani kabisa unalifahamu kusudi la wewe kuwepo hapa duniani. Hujazaliwa kwa bahati mbaya, kila mwanadamu amekuja na uwezo ambao anatakiwa autumie hapa duniani ili aweze kuishi Maisha bora na yenye mchango kwa wengine […]

HATUA YA 262:  Mambo 5 yatakayokufanya Uendelee Kubakia Hapo Ulipo.

Mara nyingi unaweza kukutana na mtu anasema “Ningekuwa na Mtaji wa shilingi fulani ningefanya biashara Fulani” sasa ukimuuliza mawazo yako ni mazuri sana sasa unafikiri huo mtaji unaousema unatoka wapi? Kuna juhudi gani unafanya sasa hivi ili angalau uwe na huo mtaji? Mtu huyo ataanza kukupa maelezo ya kutosha kwanini haiwezekani na hali ilivyo mbaya. […]

HATUA YA 261: Ni Kweli Huna Muda?

Ukiona mtu anakwambia hana muda au yuko bize sana wala usiumize kichwa sana unatakiwa ujue kwamba huyo mtu hajaamua kulipa lile jambo lako kipaumbele au hajaamua kukupa wewe kipaumbele. Inawezekana mtu ana majukumu mengi sana ya maisha yake kiasi kwamba anashindwa kufanya mambo mengine ambayo anapaswa kuyafanya kweli lakini pale linapokuja swala la msingi katika […]

HATUA YA 260:  Vitu Hivi Unavyoviruka Vitakutesa Baadae.

Kuna michezo kama hukuicheza ukiwa mdogo huku ukubwani itakuja kukusumbua. Hili lina ukweli wake kiasi Fulani japo sio kwa mambo yote. Tukija kwenye upande wetu wa maisha kuna mambo ambayo unaweza kukutana nayo na ukayaona ni magumu bora uachane nayo. Ukweli ni kwamba huko baadae yatakuja kukusumbua. Kuna sehemu utashindwa kuzifikia kwasababu ya hatua ulizoziruka. […]

HATUA YA 259: Ni Dharau au Ni Hisia Zako.

Nimezoea kuona watu wengi ambao wako chini kwenye vitu Fulani kuwaona wenzao waliowapita kama wana dharau sana. Mfano mtu mwenye bodaboda atasema watu wenye magari wana dharau na hawawajali bodaboda. Vilevile maskini ataona matajiri wengi wana dharau, wanajisikia, wanajiona, hawawapendi maskini. Ni wachoyo na mengine mengi. Kama na wewe umeshakuwa na hisia kama hiyo kuona […]