HATUA YA 262:  Mambo 5 yatakayokufanya Uendelee Kubakia Hapo Ulipo.

Mara nyingi unaweza kukutana na mtu anasema “Ningekuwa na Mtaji wa shilingi fulani ningefanya biashara Fulani” sasa ukimuuliza mawazo yako ni mazuri sana sasa unafikiri huo mtaji unaousema unatoka wapi? Kuna juhudi gani unafanya sasa hivi ili angalau uwe na huo mtaji? Mtu huyo ataanza kukupa maelezo ya kutosha kwanini haiwezekani na hali ilivyo mbaya. […]

HEKIMA YA JIONI -2

Ukisema unangoja mambo yawe mazuri ndio ufanye biashara, au ununue kitabu, au uanze kile kitu ulichokuwa unakitaka nikwambie ukweli unajidanganya. Kama hiyo hali mbaya uliyonayo sasa hivi haijaweza kukufanya ufanye maamuzi ya kuanza kile unachokitaka usitegemee hali ikiwa nzuri ndio utachukua hatua. Zaidi sana hali ikiwa nzuri ndio utasahau kabisa hata kama kuna watu huwa […]

HEKIMA YA JIONI-1

Watu wengi wamekuwa waoga hasa pale wanapojilinganisha na wengine na kujiona wao ni wa kawaida na hivyo kushindwa kujitambulisha vyema wanapokutana na wengine. Unaweza kufanya makossa ukapoteza wateja wapya ambao ungewapata kwa kusema tu unachokifanya, hata kama huna ofisi usiogope kusema unafanya biashara gani. Kuwa Mfuasi wa Kwanza wa Ndoto zako, usisubiri hadi watu waanze […]

HATUA YA 260:  Vitu Hivi Unavyoviruka Vitakutesa Baadae.

Kuna michezo kama hukuicheza ukiwa mdogo huku ukubwani itakuja kukusumbua. Hili lina ukweli wake kiasi Fulani japo sio kwa mambo yote. Tukija kwenye upande wetu wa maisha kuna mambo ambayo unaweza kukutana nayo na ukayaona ni magumu bora uachane nayo. Ukweli ni kwamba huko baadae yatakuja kukusumbua. Kuna sehemu utashindwa kuzifikia kwasababu ya hatua ulizoziruka. […]

Sifa 5 za Mtu Anaelekea Kwenye Mafanikio Makubwa.

Habari za Leo Rafiki na Mwanamafanikio mwenzangu. Ni matumaini yangu kwamba unaendelea vyema na afya pamoja na safari hii ya mafanikio. Siku zote napenda kukwambia kamwe usikate tamaa. Haijalishi ni magumu kiasi gani unapitia sasa. Ipo siku Matokeo ya unachokifanya yatakuja kuonekana. Leo tujifunze juu ya Sifa tano ambazo zinaonyesha mtu huyu anaelekea Kwenye Mafanikio […]

HATUA YA 259: Ni Dharau au Ni Hisia Zako.

Nimezoea kuona watu wengi ambao wako chini kwenye vitu Fulani kuwaona wenzao waliowapita kama wana dharau sana. Mfano mtu mwenye bodaboda atasema watu wenye magari wana dharau na hawawajali bodaboda. Vilevile maskini ataona matajiri wengi wana dharau, wanajisikia, wanajiona, hawawapendi maskini. Ni wachoyo na mengine mengi. Kama na wewe umeshakuwa na hisia kama hiyo kuona […]

HATUA YA 258: Moyo Wako Uko Wapi?

Mojawapo ya sababu ambazo zinawafanya watu waharibu kazi za wengine ni kufanya kazi huku mioyo yao iko sehemu nyingine kabisa. Wewe umekuwa mwalimu kwasababu uliona ndio utapata kazi kirahisi lakini moyo wako uko kwenye kilimo siku zote utakuwa ni mwiba kwa wanafunzi. Biashara nyingi zimekosa maendeleo n ahata mafanikio kwasababu ya hawa watu ambao wanafanya […]

HATUA YA 257: Kuna Mtu Katoka Jasho.

Kuna msemo wa wahenga unasema ukiona vyaelea ujue vimeundwa. Yaani chochote kile unachokiona kimependeza kwa nje unatakiwa ujiongeze kwamba kuna watu tena inawezekana wasiojulikana wamekifanyia kazi kwa wakati usiojulikana hadi kikaanza kuonekana kwa nje ni kizuri. Sasa wewe kwa tamaa zako unataka ukipate kile ambacho wenzako wamekifanyia kazi kwa muda mrefu sana hadi ukaanza kuvutiwa […]

HATUA YA 256:  Dunia Inakuhitaji?

Ni vyema kujiuliza na kujijibu kama kweli dunia inakuhitaji uendelee kuwepo hapa duniani. Lazima ujiulize hivi siku ukiondoka ni wakina nani wataguswa sana na kifo chako? Ili ujue ni kwa kiasi gani unahitajika hapa duniani lazima utambue ni thamani gani unatoa kwa dunia. Ni vitu gani vinatoka ndani yako na vinaleta matokeo na mabadiliko hapa […]

HATUA YA 255: Unataka Kwenda Hatua Nyingine?

Unataka Kwenda hatua ya juu Zaidi? Lazima ukubali kupitia mitihani ya kukupima kama unaweza kukaa kwenye hatua inayofuata. Kama hutaki kupita kwenye mitihani huwezi kupanda hatua nyingine. Kama hutaki kupimwa hutaweza kuingia kwenye hatua za juu Zaidi utabaki hapo ulipo kwa muda mrefu Zaidi. Ukiona unabaki sehemu moja muda mrefu kuna uwezekano kuwa unafeli mitihani. […]