HATUA YA 292: Ni Rahisi Sana Lakiniā€¦

Ni rahisi sana kulalamika Maisha ni magumu, Ni rahisi sana kutoa sababu nyingi zilizofanya ushindwe, Ni rahisi sana kuendelea kuishi Maisha yale yale uliyoyazoea, Ni rahisi sana kutumia muda wako kufanya mambo ambayo hayana mchango wowote kwenye Maisha yako. Ni rahisi sana kutumia muda wako kufuatilia Maisha ya wengine na huku ukiwa umeyasahau ya kwako. […]

KAMA UNA SIFA HIZI WEWE NI MJASIRIAMALI

Habari za leo mwanamafanikio. Leo ninataka kukuonyesha mambo machache ambayo yanaonyesha wewe ni Mjasiriamali. Katika dunia ya sasa tunahitaji watu wengi ambao ni wajasiriamali watu ambao wako tayari kuchukua hatua kubadilisha Maisha ya wengine pamoja na ya kwao wenyewe. 1.Decision maker (Mfanya Maamuzi) Kama wewe una uwezo wa kufanya maamuzi linapotokea jambo mbele yako bila kusita […]

HATUA YA 270: Wanakupenda sana ila wanakuharibia Bila Kujua.

Kama ukipata tatizo lolote kwenye maisha yako kuna sehemu ukienda ukajieleza tu unaeleweka na tatizo lako linatatuliwa unaweza kufikiri kwamba upo sehemu nzuri sana. Ukweli ni kwamba upo sehemu ya hatari kuliko nyingine yeyote kwenye maisha yako. Ni rahisi sana mtu kupenda pale ambapo akipeleka matatizo yake yanatatuliwa. Ni hatari sana kama hayo matatizo ulipaswa […]

HATUA YA 269: Huhitaji Kikubwa Sana.

Mara nyingi tunafikiri ili ufikie hatua kubwa kwenye maisha lazima uanze na mwanzo ambao ni mkubwa sana. Usifikiri kwamba ukiwa na vitu Fulani na Fulani basi ndio maisha yako yatakwenda vizuri. Kama umeshindwa kutumia rasilimali ulizonazo sasa hivi hata ukipewa kubwa bado utashindwa na unaweza ukaharibu badala ya kutengeneza. Uwezo wako unapimwa kwa namna ambavyo […]

HATUA YA 268: Swali La Kujiuliza Unapojua Unachokitaka.

Kujua kile unachokitaka ni jambo la kwanza, kinachofuata ni kufahamu gharama ambazo unapaswa kulipa ili kufika pale unapotaka. Wengi wanaishia kwenye kujua wanachotaka na kukata tamaa baada ya kuambiwa gharama wanazotakiwa kulipa.   Ni vyema ukajiuliza maswali haya na ukapata majibu yake wakati unaanza safari yako. Unajua gharama gani unapaswa kulipa ili ufike unakotaka kwenda? […]

HATUA YA 267: Nipo Hapa tangu 96!

Siku moja nikiwa maeneo ya stand nikakutana na watu wawili wakigombania Tsh elfu mbili mmoja katika hasira sana akamwambia mwenzake wewe mbona unakuwa kama umekuja stand jana? Kwa hasira sana mwenzake akajibu kwamba nipo hapa tangu mwaka 96 nikashangaa sana kuona watu sh elfu mbili inawafanya wajivunie kuwepo kwenye kitu kile kile bila ya mabadiliko […]

HATUA YA 265: Mambo Yakufanya Ili Kuacha Tabia Mbaya yeyote.

Yafanya wasiwe na maisha bora na mojawapo ya hayo mambo ni tabia mbaya. Tabia hizi nyingi zimekuwa ni tatizo kwenye maisha ya watu kwani kuziacha imekuwa ni tatizo sana. Tabia nyingi mbaya huanza kujengeka kidogo kidogo na mwisho wake zinakuwa ni kama ulevi kwenye maisha yetu. Ni hatari sana kama utashindwa kufanya namna kuziacha kwani […]

HATUA YA 264: Unakuwa Kile Unachoamini.

Unakuwa Kile unachokiamini, kuamini kunakuja kwa kupitia njia mbalimbali kwanza ni kusikia, kuona, na wakati mwingine kusoma. Tukianza na kusikia kama akili yako na ufahamu wako utakuwa umeupa nafasi ya kusikia mambo mazuri yanayoendelea utajenga Imani ya mambo mazuri. Kama utaipa nafasi ya kusikia mambo mabaya yanayoendelea utajenga Imani ya kwamba kuna hali mbaya sana […]

HATUA YA 263: Vile Usivyotaka Kuonekana.

Kuna aina Fulani ya maisha ambayo mara nyingi unapenda watu wajue kuwa unayo au unayaishi lakini katika uhalisia hauishi maisha hayo. Ni kwekli sio sawa kuonyesha kila kitu wazi kwenye dunia lakini ni vyema sana yale maisha ambayo unataka watu waone na wajue kuwa unayaishi ukaanza kuyaishi kiuhalisia badala ya kujifanya. Ukiendelea kujifanya kuwa una […]

BARUA MAALUMU KWA VIJANA AMBAO BADO HAWAJAOA AU KUOLEWA.

Habari za leo Rafiki, ni matumaini yangu kila mmoja anaendelea vyema kwenye Maisha yake na kupambana ili kupata matokeo bora Zaidi. Nina Imani kabisa unalifahamu kusudi la wewe kuwepo hapa duniani. Hujazaliwa kwa bahati mbaya, kila mwanadamu amekuja na uwezo ambao anatakiwa autumie hapa duniani ili aweze kuishi Maisha bora na yenye mchango kwa wengine […]