HATUA YA 30: Hivi ni Vitu vya Msingi kama unataka kudumu kwenye Mafanikio.

Kama kuna sehemu utakosea ni kusahau kujali vitu vya muhimu sana kwenye Maisha yako wakati unatafuta mafanikio na mali za ulimwengu huu. MAHUSIANO; Wakati unatafuta pesa usijisahau ukaacha kutengeneza mahusiano mazuri na familia au wale unaowapenda. Unaweza kutafuta pesa nyingi sana kwenye dunia hii kisha unashindwa kuja kuzifurahia kwasababu wale unaowapenda na waliokupenda uliwasahau hivyo […]

HATUA YA 29: Sio Kila Vita Upigane wewe!

Kuna baadhi ya watu huwa unawakuta kwenye kila kitu. Kila kinachokuja kipya anakuwepo ndani yake. Kila fursa mpya unayotokea unataka ufanye. Mafanikio hayatakuja kwa kufanya vitu vingi bali kwa kufanya mambo machache hadi yakakuletea matokeo. Jifunze kufanya jambo moja hadi lilete matokeo. Nikwambie ukweli kama unachokifanya sasa kuna watu wanaendelea kukifanya na wana mafanikio makubwa […]

HATUA YA 28: Unaweza Kutoka hapo Ulipo.

Haijalishi upo kwenye hali gani sasa bado unayo nafasi ya kusimama tena. Inawezekana ulishasema haiwezekani lakini leo nina neno kwa ajili yako. Unaweza kufanya mambo makubwa sana. Njia za wewe kufanikiwa zinaendelea kufunguka kila, ni  wewekufungua macho na kuziona. Ili utoke hapo ulipo ni lazima uamue kuchukua hatua ya kubadili Maisha yako. Lazima ukubali kufanya […]

HATUA YA 27: Acha Kujikataa,

Pale inapofika wakati ukaanza kujiona huwezi vitu Fulani kwasababu ya elimu yako ndogo unapoteza uwezo wako mkubwa taratibu. Kuna maneno ambayo ni hatari sana kujitamkia kwenye Maisha yako kwani yanakuharibu kabisa. Yanakufanya ushindwe kwenye kila jambo unalofanya. Haya; Mimi sina Elimu ya Kutosha hivyo hii biashara siiwezi! Kwetu ni maskini sana hakuna hata mmoja tajiri! […]

HATUA YA 26: Tatizo sio Pesa Tatizo ni Wewe,

Tatizo sio kwamba huna pesa tatizo ni fikra zako juu ya pesa zilivyo. Unafikiri kwamba siku ukipata pesa utafanya hivi na hivi. Ukweli ni kwamba pesa unazipata kila siku lakini hujui. Ukibadili unavyofikiri juu ya pesa utakuwa umebadili matatizo yako ya kipesa yote. “The greatest of evils and the worst of crimes is poverty… our […]

HATUA YA 25: Huyu ndie anaekuweka Mjini,

Kama ulikua hujui kwenye hii dunia kila binadamu anauza. Kila mtu kuna kitu anauza au kama hauzi basi hajajua kama anauza. Unatakiwa ujue ni kitu gani hasa unakiuza ili uweze kukiuza vizuri. Unatakiwa ujue unaemuuzia ni mtu wa namna gani! Hata kama una bidhaa nzuri kiasi gani kama humjui mteja wako huwezi kuuza vizuri au […]

HATUA YA 24: Kwanini Ulizaliwa Mwanadamu?

Leo nataka ujiulize kwanini Mungu alikuumba wewe mwanadamu na wala sio kiumbe kingine chochote? Ukijua hivyo huwezi kujidharau! Ukijua hivyo huwezi kujifananisha na wengine! Ukijua hivyo huwezi kukubali kushindwa! Ukijua hivyo huwezi kukata tamaa kirahisi! Utajua unapoelekea! Utajua watu wakuambatana nao!  Utajua ni vitu gani vya Kusoma! Mnyama wa kawaida hua anawaza vitu viwili tu […]

HATUA YA 23: Unataka kwenda Mbali au Unataka Kufika Haraka?

Kuna msemo mmoja unasema kwamba “Kama unataka kufika haraka nenda/tembea mwenyewe. Kama unataka kufika mbali usiende peke yako nenda pamoja na wengine.  “If you want to go quickly, go alone. If you want to go far, go together.” Ukienda peke yako Hutafika mbali, hutaenda mwendo mrefu utachoka. Kama safari yako ni ndefu usichague kwenda peke […]

HATUA YA 22: Unacho cha Kupoteza?

Katika Maisha kuna mambo mengi sana huwa yanajitokeza na yanatufanya tuwe na hali za furaha au wakati mwingine hasira. Juzi wakati nasafiri kwenda Mwanza, kwenye bus kulikuwa na mtu alilipa akaa kwenye siti mbele ya safari akaja kuambiwa ilikuwa na mtu tayari yupo kituo cha mbele hivyo asimame. Pale ndani ya gari kukatokea mabishano makubwa […]

HATUA YA 46: Ukweli Utakuweka Huru.

Kuna msemo mmoja unasema ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu. Walisema hivi kwa sababu ukidanganya halafu ukasahau ulichodanganya huwezi kuwa huru. Ukidanganya mara ya kwanza itakubidi udanganye mara ya pili. Uongo ni tabia mbaya sana ndio maana ulipokuwa mdogo ulichapwa sana pale ulipodanganya. Ukweli Utakuweka Huru kwa sababu huna haja ya kukumbuka ulichokisema. Mara zote unapokuwa […]