HATUA YA 21: Tafuta Muda Mzuri na Wewe Peke Yako.

Ni Mara ngapi umekuwa ukiwapa watu muda wako? Ni mara ngapi umekuwa ukivipa vitu vya namna mbalimbali kwenye Maisha yako?   Umekuwa ukitumia muda mwingi na Tv au marafiki lakini ukasahau kutumia muda na wewe mwenyewe. Umekuwa unatumia muda mwingi kazini kwako na kwenye shughuli zako nyingine lakini hupati nafasi ya kukaa na wewe pekee […]

HATUA YA 3 : Hapo Ulipo Sasa.

Hapo ulipo sasa usipadharau na kujiona upo nyuma sana. Kuna wengi sana wanatamani wafikie HATUA uliyofikia wewe. Kuna wengi wanajifunza kwa HATUA uliyofikia leo. Hata kama huoni wanaokupongeza kuna watu wanajifunza mno juu ya kile unachokifanya. Ninasema hivi Kwasababu inawezekana umekata tamaa na kujiona uko chini na wakati Mwingine kutokujali kile ulichonacho sasa. Kijali sana […]

HATUA YA 20: Andika Historia.

Kila hatua unayopita hakikisha huachi hivi hivi, Hakikisha uneacha alama. Ni changamoto unapitia Hakikisha haikuachi hivi bure, utoke na cha kujifunza, Hakikisha Unatoka na hadithi Nzuri ya kuwaeleza watu. Maisha yetu yamefungwa kwenye muda, kadiri tunavyotumia muda ndio tunavyomaliza kuishi. Kila unachokifanya Hakikisha kinaacha alama. Watu unaokutana nao Hakikisha unawaacha wakiwa wa tofauti. Hakikisha unawaachia kitu […]

HATUA YA 2: Unahitaji au Unajionyesha?

Nunua kitu Kwasababu unakihitaji sio kwa ajili ya kuwaonyesha wengine kwamba una uwezo wa kipesa. Tatizo kubwa linalotusumbua ni kwamba tunafanya mambo ili watu watuone. Mtu ananunua mavazi ya gharama sio Kwasababu anayahitaji bali ni ili watu wajue ana uwezo wa kipesa. Mwingine ananunua gari jipya ili watu waone sio Kwasababu ya mahitaji yake. Ukiwa […]

HATUA YA 19: ASILI HAIBADILIKI.

Mojawapo ya vitu ambavyo havitaweza kubadilishwa ni vile ambavyo aliviumba Mungu. Lakini kila alichogundua mwanadamu unaweza kufikiri namna ya kukiboresha. Mwanadamu ukisema umuongezee kiungo kingine unaharibu mfumo mzima au hawezi kuwa sawa na wanadamu wengine. Huwezi kubadili chochote kinachotokana na asili. Waliojaribu kutuletea vitu ambavyo ni vya asili wakajaribu kurekebisha vinaleta madhara makubwa kwenye Maisha […]

HATUA YA 1. Kupiga Hatua Kuna Gharama.

Kwenye safari yetu ya mafanikio kuna vitu vingi tunafanya ili tusonge mbele kila wakati. Ili mtu atoke sehemu moja aliyokuwepo na kusogea mbele anahitaji kulipa gharama. Sio kitu kirahisi kama unavyoweza kufikiri ndio maana sio wote wanaweza.  Watu wengi huingia kwenye biashara au huanza vitu vipya na kutegemea matokeo bila kulipia gharama yeyote. Kama ilivyo […]

HATUA YA 18: Usiishie Njiani.

Heri Ya Mwaka Mpya. Nina neno moja tu kwako mwaka huu wa 2017. #USIISHIE NJIANI. Yapo mengi sana Ulianza mwaka jana ukaweka malengo makubwa lakini ukaishia njiani. Mwaka huu sio wa kuishia njiani. Mwaka huu ni wa kumaliza ulichokianza. Mwaka huu ni wa kufikia mafanikio makubwa. Mwaka 2017 ni wa kwako wa Kupiga hatua. Mwaka […]

HATUA YA 17: Tafuta mtu wa Kukukosoa.

Wanadamu kwa asili tunapenda kusifiwa. Pale inapotokea mtu amekukosoa wakati mwingine unaweza kufikiri anakuonea wivu au vingine. Lakini ukweli ni kwamba hatuwezi kukua au kuwa bora bila kupitia changamoto hii ya kukosolewa.Mwandishi huyu anasema “Mjinga yeyote anaweza kukosoa, kulaani, na kulalamika lakini inahitajika tabia na kuweza kujidhibiti ili kuelewa na kusamehe. ~ Dale Carneige Kwenye […]

HATUA YA 16; Noa Shoka Lako.

Usiparamie mti wakati shoka ni butu. Utatumia nguvu kubwa sana lakini utapata matokeo madogo. Abraham Lincoln aliwahi kusema kwamba akipewa masaa sita kukata mti atatumia masaa manne kunoa shoka lake. Hii inatufundisha kwamba ni muhimu sana kujiandaa vyema kwa kile unachotaka kufanya. Hii haimaanishi kwamba uchelewe kuanza kwa kisingizio unanoa shoka. Au unajiandaa. Chochote unachotaka […]

HATUA YA 15; KUFIKIRI NA KUTENDA.

Kufikiri na kutenda ni vitu viwili ambavyo huwa haviachana popote utakapofanya jambo. Mambo mengi mabaya na mazuri hua yanatokea hapa duniani kwasababu ya hivi vitu viwili. Ukitenda bila kufikiri utapata matokeo mabaya sana. Ukifikiri bila kutenda utabaki bila matokeo yeyote. Haijalishi umefikiri vyema kiasi gani usipoweka kwenye matendo hakuna matokeo utakayopata. Kufikiri bila kutenda kunasababisha […]