401; Kila Kitu Kilianza Kama Wazo.

Tangu mwanzo wa kuumbwa kwa ulimwegu huu kila kitu kilianza kama wazo. Mungu alikaa akawaza kuleta uhai katika sayari ya dunia baada ya sayari hii kuwa imejaa maji pekee yake. “Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu” (Mwanzo 1:26). Na hakuishia hapo vitu vingine vyote ambavyo unaviona havikutokea tu vyenyewe bali vilitokana na mawazo yake mwenyewe. Kitu […]

Ni wewe Mwenyewe Umechagua 18/11/2018.

“Mwaka 2016 tulikuwa kwenye msiba wa jirani yetu ambaye alifiwa na mama yake. Siku hiyo watu walikuwa wanalia sana na kusikitika kwa kifo kile kilichotokea. Kitu kimoja ambacho kilimshangaza kila mtu ni kwamba mtoto wa kiume wa marehemu alikuwa hana machozi na wala hana huzuni sana kama ambavyo wengi walidhani itakuwa hivyo. Watu wakajikuta wanajiuliza […]

VITU 5 UNAVYOPASWA KUVIFAHAMU ILI UWEZE KWENDA NA KASI YA MABADILIKO-9/11/2018

Tupo kwenye dunia ambayo kila kukicha kunakuwa na mabadiliko mapya katika sehemu mbalimbali hasa za kiteknolojia. Kama mwanadamu ukishindwa kwenda na kasi hii kuna mambo mengi utajikuta unashindwa kufanya au unalipa gharama kubwa sana ili tu yafanyike. Kuna vitu vingi ambavyo ungevijua vingeweza kuwa rahisi sana kwako kugundua fursa mbalimbali ambazo zingekuingizia kipato. Kwasababu hujafahamu […]

Usisubiri Hadi Ujisikie Vizuri-8/11/2018

Ni kweli hakuna kuchelewa katika mafanikio yaani hata kama una miaka 60 sasa hivi bado unaweza kuchukua hatua na kuitimiza ndoto yako. Wapo pia watu wanasema kama umepangiwa kufanikiwa utafanikiwa tu, kama umepangiwa kuwa maskini utakuwa masikini hata upambane vipi. Hayo ni aina ya mawazo ambayo unaweza kuwa nayo na yakawa sababu ya wewe kuendelea […]

Hutaondoka Ukiwa Hai -3/11/2018

Kwa vyovyote vile hata kama utaogopa kufanya mambo yaliyo makubwa, hata kama utaogopa kupoteza pesa zako bado huwezi kuondoka duniani ukiwa hai. Kama unaogopa kupata msongo wa mawazo kwasababu biashara itakusumbua Rafiki yangu hata usipoupata huo msongo wa mawazo bado hapa duniani utaondoka ukiwa umekufa. Hatujui ni kitu gani kitakuondoa duniani hivyo basi wewe endelea […]

Kufanikiwa au Kufa-2/11/2018

Kama unafikiri kutafuta pesa ni ngumu basi jaribu kukaa bila pesa uone ilivyo rahisi. Naomba nikwambie Rafiki mafanikio sio lelemama yaani sio kitu ambacho kinakuja chenyewe tu lazima uweke juhudi za kutosha. Lazima uwe na nidhamu ya kutosha. Wewe usifikiri ni kama vile ambavyo umeshajizoesha. Kuna vitu vya ziada ambavyo unatakiwa kuvifanya na hujazoea kuvifanya […]

Kufanikiwa Au Kufa 1/11/2018

Ukitaka vitu vya tofauti ni lazima ukubali kufanya vitu ambavyo hujawahi kufanya. Kama unataka kufanya vitu ambavyo hujawahi kufanya lazima ukubali kufanya maamuzi magumu ambayo hata watu wa karibu wanaokutazama wanaweza kuogopa. Kama utaendelea kubaki hivyo ulivyo na ukafanya unayoendelea kufanya kila siku maana yake utapata matokeo yale yale na hutasogea mbele hata kidogo. Wanajeshi […]

26/10/2018 Maisha Yako Ya Sasa Ni Matokeo ya Kitu Hiki..

Aliwahi kusema Charlie Jones kwamba utakuwa mtu yule yule miaka mitano ijayo isipokuwa watu utakaokutana nao na vitabu utakavyosoma. Hii ina maana kwamba kama utaendelea kubaki na vitu vile vile ambavyo umekuwa unavifanya utaendelea kubaki vile vile. Hii pia ina maana kwamba maisha yako ya sasa ni mchango wa watu ambao umekutana nao miaka 5 […]

25/10/2018 Uepuke Mtego Huu Uliowaangusha Wengi.

Unapokuwa huna chochote cha thamani huwezi kuona mtu yeyote akionesha kuvutiwa na wewe. Wakati mwingine unaweza kuwa unafanya mambo ya maana sana lakini ukashangaa hakuna mtu anahangaika na wewe. Hakuna mtu atahangaika na wewe kama ulichokibeba hakina thamani. Hakuna mtu atapoteza muda wake kwako kama wewe huna cha maana ulichobeba. Unapoanza kuona unapata marafiki wapya, […]

400: Hakuna AnaeKulazimisha.

Ulipokuwa mtoto kuna nyakati ulikuwa ukichelewa kuamka unakuja kuamshwa na viboko au wakati mwingine unamwagiwa maji. Kuna wakati pia ulikuwa unalazimishwa kusoma kwa bidii na unaambiwa uweke maji kwenye beseni ili usisinzie. Naomba ujiulize hivi sasa ni nani tena anaekulazamisha tena ufanye kazi kwa bidii ili uwe na pesa? Ni nani tena anaekuja kukuamsha mapema […]