Ni bora mara elfu kukaa ndani peke yako kuliko kuambatana na marafiki wapumbavu. Ni bora kuishi ndani ya nyumba peke yako kuliko kujichanganya na makundi yasiyofaa.

Haijalishi una maono makubwa kiasi gani, au ndoto kubwa kiasi gani unaweza kuharibu mwelekeo wako kwa kupitia aina ya makundi unayoambatana nayo. Kuna watu hawakufai hata kidogo kwenye maisha yako.

Kuna aina ya watu ukionekana nao tu hata wale watu ambao wangetaka kukusaidia vitu Fulani wanaogopa maana wanajua utakuja kuwaangusha.

Kuna aina ya watu ukiambatana nao watu wanabaki na maswali kichwani sasa huyu tukimkaribisha hapa nyumbani si atatuletea wezi huyu.

Kuna aina ya watu ambao hawasomi vitabu wao kila kukicha wako bize na movie pamoja na starehe hawa ukiwa nao lazima upotee.

Kuna aina ya watu ukiwa nao siku zote wakipata pesa wanawaza starehe tu, hawa lazima ukae nao mbali maana watakuambukiza tabia zao.

Kuna aina ya watu wana maono makubwa, ndoto kubwa lakini wanakosa vitu vichache hawataki kujifunza, ukiwaambia kuanzia chini hawataki wanaona aibu wao wanasubiri mtaji au mtu mkubwa aje awape mtaji. Hawa kaa nao mbali watakuchelewesha kwenye safari yako.

Kuna aina ya watu ambao wakiwa na mambo yao wanataka uwasikilize, uache mambo yako, uairishe ratiba zako kwasababu tu wao wana jambo lao la muhimu. Lakini sasa wao hawajawahi kukusikiliza hata siku moja. Hawajawahi kuacha mambo yao kwa ajili yako hata siku moja. Hawa waepuke kabisa wanakunyonya nguvu zako.

Kuna aina ya watu ambao wanafanana na wewe kila kitu wanasoma kwa bidii wana ndoto kubwa na wanajua wanchokifanya. Kuna kitu au vitu wanafanya kila siku ili kufikia ndoto zao. Hawa usiwe nao wengi sana angalau wawili au watatu tu wanakutosha.

Tengeneza watu wenye mafanikio makubwa kuliko wewe ambao watakuwa ni marafiki zako. Hawa sio watakusaidia kifedha tu hapana watakuelekeza hata sehemu ambazo unakwama jinsi gani ya kuvuka. Hawa wanaweza kukupa msaada wa watu wa kukusaidia sehemu mbalimbali ili utoke kimafanikio.

Ukikosea kwenye kuambatana na watu utapotea kabisa. Usijidanganye eti wewe utambadilisha kazi yako sio kubadilisha watu tuachie sisi tunaohamasisha na kuandika tuwafundishe.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading