#USIISHIE_NJIANI: Hali Mbaya Uliyonayo Inasababishwa na Hiki

Leo jioni nikiwa nazishika ndevu zangu ghafla katika fikra yakanijia maneno ambayo niliambiwa miaka karibia kumi iliyopita. Kuna mtu mmoja aliniambia “wewe ukiwa na ndevu utakuwa mbaya sana”. Nikabaki najiuliza kwanini haya maneno yamekuja sasa hivi wakati nashika ndevu? Mbona ni muda mrefu sana umepita na nilishayasahau kabisa? Nikagundua kwamba maneno uliyonenewa na watu yanabaki […]

#USIISHIE_NJIANI: Wewe Sio Mti.

Mti unapokuwa kwenye mazingira ambayo hayasababishi mti usitawi unakuwa hauna namna yeyote ya kubadilisha mazingira yale ili uendelee kukua. Mara nyingi kinachotokea baada ya mti kuwepo sehemu ambayo haina rutuba na pia haina maji ni kukauka au kupambana na hali hiyo mwishoe ni kudumaa. Sasa wewe rafiki yangu sio mti, kama mazingira uliyopo yanakunyima fursa […]

#USIISHIE_NJIANI-  Jawabu la Unachokitaka ni Hili hapa.

Penda kujipa muda wa kusubiri matokeo unayoyataka wakati unayafanyia kazi. Bahati mbaya hatuna kipimo maalumu cha muda ili uwe na uhakika wa unachokisubiria. Kama mwanamke amebeba ujauzito inafahamika kabisa ni baada ya miezi tisa atajifungua. Na endapo itatokea tofauti na hapo muda ukizidi tunaanza kupata wasiwasi. Kwenye mafanikio hakuna mahesabu ambayo yapo na uhakika kabisa […]

#USIISHIE_NJIANI- Kujionyesha na Uhalisia.

Haina maana yeyote kama watu watajenga picha kubwa kwako kutokana na namna unavyopenda kujionyesha halafu uhalisia ukawa ni tofauti kabisa. Ni vizuri sana ukaishi vile unavyopenda lakini ni vyema ukakubali kulipa gharama za hayo maisha kwanza ndipo uje kufurahia baadae. Ni kichekesho sana kama utakuwa unatamani watu waone unaishi maisha mazuri wakati kwa ndani unateseka […]

#USIISHIE_NJIANI: UTAONDOKA PEKE YAKO.

Habari rafiki. Kitu ambacho hupaswi kukisahau ni kwamba hapa duniani ipo siku utaondoka. Na kitu cha kukumbuka Zaidi ni kwamba utaondoka peke yako. Wale wote uliokuwa unawaonea aibu, unaona kwamba watakusema vibaya, wataona umejishusha hadhi kwa kufanya kile unachokitaka hutaondoka nao. Inawezekana ukawaacha duniani au wakakutangulia. Sasa nikwambie rafiki hii ni dunia kila mmoja alikuja […]

#USIISHIE_NJIANI: JIPE MUDA.

Habari Rafiki. Chochote unachokifanya sasa hivi kabla hujaanza kukata tamaa hakikisha umejipa muda wa kutosha. Jipe muda ambao utafanya kazi kwa bidi, utajenga mtandao mkubwa wa watu wanaofahamu unachokifanya. Jipe muda wa kujifunza na kuona kule unakotaka kufika. Shida kubwa ipo kwa watu wasio na maono makubwa wanataka pesa za haraka. Unaanza biashara au wazo […]

USIISHIE NJIANI: Siri Ya Mafanikio (Hakuna Mwendokasi)

Kitu chochote kinachopatikana haraka hasa kitu kikubwa sana mara nyingi yule anaekipata hushindwa kukihimili. Hasa tukiangalia upande wa fedha na utajiri tunaweza kuwa na mifano mingi sana ya watu ambao walipata fedha nyingi ndani ya muda mfupi na wakaishia kuwa maskini kama zamani. Unajua mafanikio ni sawa na mtu anaepanda juu kwenye kilele cha mlima. […]

#USIISHIE NJIANI: HAKUNA NJIA MOJA AMBAYO NI SAHIHI.

Habari rafiki, Umeanzaje siku yako? Umefanya mazoezi? Umesoma kitabu? Ukweli ambao unaweza kuwa hupendi kuusikia ni huu, hakuna njia moja ambayo ni sahihi ukiifanya lazima ufanikiwe. Hakuna biashara ambayo ndio sahihi lazima ukiifanya ufanikiwe. Kila biashara kuna waliofanikiwa Zaidi, wa kawaida na waliofeli na wengine wanajuta kabisa kufanya biashara hiyo. Hivyo rafiki yangu usikae mahali […]

#USIISHIE_NJIANI: VIGEZO NA MASHARTI

Habari ya asubuhi Mwanamafanikio. Tumeanza tena wiki siku ya leo. Hakikisha umeipanga wiki yako ili uweze kuwa na matokeo bora. Jua ni vitu gani unakwenda kukamilisha wiki hii kbala haijaanza panga ratiba zako vizuri la sivyo watu wengine watakuja na ratiba zao na wewe utaingia humo. Mwisho wa siku mambo yako yanakuwa hayaendi. Nadhani kila […]

#USIISHIE_NJIANI: BINADAMU NDIVYO WALIVYO.

Habari rafiki, Umeanzaje siku yako? Umefanya mazoezi? Umesoma kitabu? Kama utakumbuka ulipokuwa mtoto mdogo kuna mambo kutokana na utoto wako ulikuwa unapenda kujaribu sana. Kama ulikuwa mtundu sana, unaweza kupanda madirishani, mara umepanda juu ya mti. Unataka kuwasha taa, na mengine mengi. Kwa kawaida unapofanya jambo la tofauti wazazi au wakubwa zako watakwambia acha, utaumia, […]